SUAMEDIA

SUA kupitia Mradi wa SANIRICE kutumia teknolojia ya kidijitali na akili mnemba katika uzalishaji wa Mpunga.

Na: Gerald Lwomile

Imeelezwa kuwa kutokana na umuhimu wa zao la mpunga kibiashara na chakula, uzalishaji wake umeambatana na matumizi holela ya mbolea hasa aina ya naitrogen ambapo kiasi kinachozidi huchangia uchafuzi wa maii na kuongeza gesi chafuzi aina ya nitrous oxide kwenye anga la dunia.

Profesa Mshiriki na Kaimu Mratibu wa Masomo ya Umahiri na Uzamivu Prof. Akwilina Mwanri wa pili kutoka kulia mstali wa mbele akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Mradi wa SUNIRICE

Hayo yamesemwa na Profesa Mshiriki na Kaimu Mratibu wa Masomo ya Umahiri na Uzamivu Prof. Akwilina Mwanri wakati akizindua mradi wa SANIRICE ambao utafanywa Tanzania Bara.

Profesa Mshiriki na Kaimu Mratibu wa Masomo ya Umahiri na Uzamivu Prof. Akwilina Mwanri akizungumza katika uzinduzi wa Mradi wa SANIRICE

Prof. Akwilina amesema utafiti utakaofanywa na mradi huo utasaidia kupunguza matumizi holela ya mbolea ili kuthibiti kiwango cha ges chafusi na kuwa kilimo endelevu cha mpunga..


Amesema Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo kitahakikisha kinatoa ushirikiano wa kutosha kuhakikisha utafiti huo unafanyika na kuleta matokeo.

“Nimefurahi sana kuona RECODA wapo katika mradi huu kwani kuna wakati tunafanya tafiti nyingi lakini tunashindwa kuzifikisha kwa wanufaika na badala yake tunaishia kwenye makabrasha na kutoa machapisho tu” amesema” Prof. Mwanri

Akitoa ufafanuzi namna mradi utakavyofanya kazi Kiongozi wa Mradi huo Dkt. Beatrice Mwaipopo amesema mradi utajikita katika kuangalia namna wakulima wa mpunga wanavyoweza kutumia mbolea zenye Nitrojeni kuzalisha mpunga na kuepusha madhara yake kwa kutumia mbolea ipasavyo.

Kiongozi wa Mradi huo Dkt. Beatrice Mwaipopo akifafanua kuhusu Mradi wa SANIRICE

Dkt. Mwaipopo ameongeza kuwa teknolojia hiyo itawawesha wakulima kujua kiwango sahihi cha matumizi ya mbolea bila kupunguza uzalishaji wa mpunga kwa kutumia mifumo ya kisasa kabisa ya kidijitali na akili mnemba.

Mradi huo unashirikisha Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, na Wakala wa mbolea TFRA, na asasi isiyo ya kiserikali inayojihusisha na usambazaji wa teknolojia kwa wakulima, RECODA.





Post a Comment

0 Comments