Na: Winfrida Nicolaus
Wanataaluma
wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) wametakiwa kujitokeza ili kuuonesha
umma na Taifa kwa ujumla maeneo yao ya umahiri na nini wamefanya na namna wanavyoweza
kuisaidia jamii ya watanzania pamoja na Chuo kupitia maeneo hayo zikiwemo tafiti
zao.
Amesema
faida ya kufanya mfululizo wa mihadhara kwa wanataaluma ni kuwasaidia kuwafahamu
watu na maeneo yao ya umahili na endapo wakiwa wanatafuta watu wa kusaidia kwenye
kazi mbalimbali chuoni hapo basi ni lazima wakafahamu nani yuko wapi na
amefanya nini.
Aidha
Dkt. Kassim amesema mwanataaluma kokote duniani anafahamika kwa ufanisi na
umahili hivyo hawawezi kufahamu ufanisi na umahili wa wanataaluma walionao kama
hawatawaita na kufanya mfululizo wa uwasilishaji wa mihadhara ya wanataaluma
hao.
“Kimsingi
tunako elekea ni kuzuri sana na kama tulivyoazimia hivi sasa tumefanya ni tabia
kwa wanataaluma hivyo tutakua tunaitana mara kwa mara na Ofisi ya Naibu Makamu
Mkuu wa Chuo Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalam imeahidi kushirikiana na
SUASA ambayo nayo imeahidi kutoa
ushirikiano na kupitia hii Taasisi itakuwa imejitangaza sana ulimwenguni na
kujulikana zaidi”, amesema Dkt. Kassim.
Kwa upande wake mmoja wa washiriki katika mhadhara huo Bi. Jenipher Tairo Mhadhiri Msaidizi kutoka Idara ya Mimea Vipando na Mazao ya Bustani SUA amesema Mihadhara hiyo ni mizuri sana kwa sababu inawapatia fursa ya wao kujua kile walichokifanya kwenye tafiti zao lakini pia matokeo ya tafiti hizo katika kuisaidia jamii na taifa kwa ujumla.
Amewahamasisha
wanataaluma kuweza kuhudhuria mihadhara hiyo kwa sababu watapata fursa ya
kujifunza zaidi kutoka kwa wengine lakini pia kujiongezea wigo wa kufahamiana
zaidi na wanataaluma wenzao katika kile wanachokifanya kwa kuwa wanaweza kufanya
vitu tofauti lakini lengo lao ni moja, kuisaidia jamii na Taifa kwa ujumla.
“ Tunaupongeza
uongozi wa Chuo kwa kuja na wazo hili na tunaomba liwe endelevu kwa sababu lina
faida sio tu kwa wakufunzi wa SUA lakini pia kwa jamii yetu maana itajua matokeo
ya tafiti zetu ni yapi na kwa namna gani zinaweza kuwanufaisha”, amesema Bi.
Jenipher.
0 Comments