Na: Siwema Malibiche
Wafanyakazi wa
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) wametakiwa kuwajibika ipasavyo katika
utekelezaji wa majukumu yao hasa ya kiutendaji yatakayo saidia kutoa huduma stahiki kwa jamii kwa maslahi ya
Chuo na Taifa kwa ujumla.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Menejimenti Rasilimali Watu na Utawala SUA Bw. Peter Mwakiluma wakati wa mafunzo ya Mfumo wa Ofisi Mtandao yaliyofanyika Chuoni hapo ambapo amewataka washiriki wote wa mafunzo hayo kuwajibika ipasavyo kwa kuzingatia uharaka ,wakati na usahihi wa kazi zao ili kuboresha huduma zinazotolewa na SUA.
Amesema
SUA imeleta mafunzo hayo ili
kurahishisha utekelezaji wa kazi ambapo
awali zilikuwa zinatumia muda mrefu mpaka kufanyika kwa maamuzi yake huku akiamini
mifumo hiyo ya kimtandao itasaidia kuepusha upotevu wa faili kwa sababu itasaidia kutambua kuwa
faili liko kwa muhusika gani na
itasimamia vizuri taratibu za
uendeshaji za kawaida.
Naye Afisa TEHAMA
kutoka Mamlaka ya Serikali Mtandao Bw. Thomas Malinga ambaye alikuwa mwezeshaji
wa mafunzo hayo, amesema mafunzo ya Mfumo wa Ofisi Mtandao utasaidia kuleta
uwazi wa kiutendaji na hata ikitokea mfanyakazi ameleta uzembe katika majukumu
yake itakuwa rahisi kumgundua endapo tu mifumo hiyo itatumika na kusimamiwa
ipasavyo.
Pia
ameipongeza Menejimenti ya SUA kwa kuona umuhimu wa matumizi ya mfumo huo
kwani yatasaidia kurahisha utunzaji wa faili na kuepusha upotevu wa karatasi
muhimu na amewataka washiriki wote wa mafunzo kuyafanyia kazi yote
waliyojifunza na amewataka kuendelea kufanya mazoezi mpaka pale mfumo huo
utakapoanza rasmi kutumiaka chuoni hapo.
Kwa upande
wao watunza kumbukumbu kutoka SUA Bi.
Salma Bwanaheri na Bw. Abel Macha washiriki
wa mafunzo hayo wameipongeza SUA kwa kuleta mafunzo ya Mfumo wa Ofisi Mtandao ambao utarahisisha ufanyaji wa kazi ikiwemo
upotevu wa barua na wameahidi kufanyia kazi kwa namna ambavyo wameleekezwa ili
kurahisisha utendaji wa kazi zao.
Mafunzo
hayo yanayoendelea kutolewa ndani ya Chuo
Kikuu cha Sokoine cha Kilimo yanawahusisha wafanyakazi wa Masijala,
Viongozi wa Menejimenti ya Chuo, Wakuu wa Idara na Makatibu Ofisi.
0 Comments