SUAMEDIA

SUA yakabidhi Miguu Bandia kwa Wanafunzi wenye Mahitaji Maalum

 

Na: TATYANA CELESTINE

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kimewezesha wanafunzi wanne wenye mahitaji maalum kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) kupata miguu bandia ikiwa ni muendelezo wa kuwawezesha wanafunzi wa chuo hicho ili kuondokana na changamoto mbalimbali zinazoweza kuwafanya kushindwa kusoma vizuri na kufikia malengo yao


Katika Picha ya pamoja Wanafunzi wa SUA mara baada ya kukabidhiwa miguu bandia (waliosimama mbele),Mratibu wa Elimu Jumuishi na Mahitaji Maalum SUA chini ya Mradi wa HEET Dkt. Thabita Lupeja (nyuma kushoto), na Muuguzi Mwandamizi kutoka Kurugenzi ya Huduma za Hospital-SUA Bi Christina Semwenda (nyuma kulia).

Akizungumza mara baada ya wanafunzi hao kukabidhiwa miguu bandia katika Hospitali ya CCBRT, Mratibu wa Elimu Jumuishi na Mahitaji Maalum SUA chini ya Mradi wa HEET Dkt. Thabita Lupeja amesema lengo la Chuo ni kuwafikia watu wenye mahitaji maalum kwa kuwapatia vifaa saidizi ikiwemo nyenzo za kusomea, kukuza maandishi kwa wanafunzi wenye uoni hafifu wakati wa ufundishaji, ujifunzaji na mitihani, kuwapatia shimesikio wanafunzi wenye usikivu hafifu na kutoa huduma stahiki kulingana na changamoto za wanafunzi wenye mahitaji maalum ili kuwawezesha kupata elimu stahiki kama wengine wasio na ulemavu,na hivyo kufanya ulemavu kutokuwa kikwazo katika kupata elimu.

                        

Dkt. Lupeja amebainisha kuwa wanafunzi wanne waliopata miguu bandia walipata changamoto hizo kabla ya kujiunga na  Chuo cha SUA mmoja kati yao amepatiwa miguu yote miwili na wengine  mmoja mmoja kutokana na changamoto zao ziliyopelekea kupitia michakato mbalimbali ikiwemo kuchukuliwa vipimo,  miguu bandia kutengenezwa kulingana na vipimo vyao, pamoja na kufanya mazoezi ili kumudu kutembelea miguu hiyo.

Aidha amesema endapo Mradi wa HEET utawaongezea fedha katika awamu nyingine wataweka kipaumbele kwa semina elekezi kwa jamii ya SUA ili kujenga uelewa juu ya elimu jumuishi na mahitaji maalum na hatimaye kuifanya SUA kuwa kitovu cha ubora katika elimu jumuishi, nyongeza hiyo ya fedha itasaidia kununua vifaa saidizi kwa wenye mahitaji maalum, kuboresha miundombinu  ya kufundishia na kujifunzia na hatimaye kuongeza ufaulu kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum.

                                

Wakizungumza mara baada ya kukabidhiwa miguu bandia wanafunzi wa kozi tofauti SUA akiwemo Bi. Domitila Mawata, Bw. Michael Karera, Bi. Tumaini Salum, Bi. Rahel Oisso wameelezea furaha na shukrani zao kwa mradi na menejimenti ya Chuo kupitia Kitengo cha Elimu Jumuishi na Mahitaji Maalum SUA wamesema hawakuwahi kufikiria kama ipo siku moja watatembea wenyewe pasi kupata msaada wa kutumia magongo, kusukumwa au kushikwa mkono hivyo  Miguu bandia hiyo imewaongezea hali ya kujiamini , kuona fursa juu yao, kuweza kushiriki katika kujipatia maendeleo kiuchumi, kielimu na hata umahiri katika kazi watakazoenda kuzifanya baada ya kuhitimu.

Mradi wa HEET ni wa miaka mitano kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia chini ya ufadhiri wa Benki ya Dunia unatekeleza ili kukuza elimu ya juu kama chachu ya uchumi mpya wa Tanzania kwa lengo la kufufua na kupanua uwezo wa vyuo vikuu kuchangia katika maeneo muhimu ya uvumbuzi, maendeleo ya kiuchumi, na umuhimu wa soko la ajira, kwa kuwekeza katika miundombinu 

 

              

Post a Comment

0 Comments