Na:
Tatyana Celestine
Ukuaji
wa mabadiliko chanya katika Sekta ya Misitu nchini umepelekea nchi ya Tanzania
kupiga hatua ambazo zinaenda sambamba na kutoa ajira milioni 3, kuzalisha
wataalamu 2,630 ambao wanasimamia misitu ndani na nje ya nchi hivyo wamewezesha
kutengwa kwa hekta zaidi ya milioni 45 ya hifadhi za misitu na uanzishwaji hekta
580,000 za mashamba ya misitu ya kibiashara na kusababisha Sekta hiyo kujivunia
katika Maadhimisho ya miaka 50 ya Mafunzo ya Taaluma ya Misitu nchini tangu
kuanzishwa kwake 1973.
Akizungumza
wakati wa Ufunguzi wa Maadhimisho hayo Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia ambaye pia ni Mbunge wa Mafia
Mhe. Omary Kipanga Octoba 1, 2024
katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) amebainisha kuwa Misitu nchini
ina faida nyingi ambapo inachukua asilimi 55 ya ardhi kwa upande wa Tanzania Bara
na kufanya misitu pekee nchini kuchangia zaidi ya asilimia nne katika pato la
taifa (GDP) , upatikanaji wa maji safi, makazi na malisho ya wanyama pori ,
uhifadhi wa udongo, ustawi wa baioanwai, urekebishaji wa hewa ya ukaa na
maendeleo ya utalii wa ikolojia.
Aidha
ameongeza kuwa umuhimu wa misitu nchini uonekana katika maendeleo ya taifa,
maendeleo ya viwanda katika kuongeza ajira na fursa za kibiashara nchini ingawa
asilimia 20 pekee ndiyo hutumika katika mazao ya misitu hivyo kuna uhitaji wa
kuangalia namna ya asilimia zilizobaki kutumika kwa kuleta tija kwa kuongeza
mnyororo wa thamani na ajira katika maeneo yao huku ikiwagusa watu wenye
mahitaji maalum na wanawake.
Mhe.
Kipanga amekipongeza Chuo Kikuu cha SUA kwa kuendelea kuongeza thamani ya
bidhaa za misitu kwa kuleta teknolojia rahisi katika maeneo ya vijijini kwa
wenye ujuzi na mitaji kama ilivyobainishwa na tafiti iliyofanywa na Wizara ya Elimu,
Sayansi na Teknolojia mwaka 2021 iliyoonesha ongezeko la thamani ghafi kuwa ni
shilingi Trilioni 4.65 ameitaka Wizara ya Mawasiliano na Utalii, Mali Asili na
Mazingira na wadau wengine wa misitu waimarishe ushirikiano na SUA kupitia
Ndaki ya Misitu kuongeza ufanisi na tija katika sekta hiyo ili kufikia malengo
makubwa kwa miaka 50 ijayo.
Naye Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Prof. Raphael Chibunda amemshukuru Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia kwa kuithamini Taasisi ya SUA kwa kutenga muda na kushiriki katika ufunguzi wa Maonesho hayo ya kihistoria hivyo watu wote wameombwa kushiriki kikamilifu katika kujifunza na kufahamu kuhusu misitu kwani SUA imekuwa kiongozi katika eneo la nchi za SADEC na Afrika Mashariki hivyo kupitia wiki hiyo wawe na sababu ya kufurahia pamoja na kujitathimini ili kuendelea kuwa Chuo kiongozi.
Naye Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu Prof. Maulid Mwatawala amesema katika miaka 50 Chuo kimekuwa na shahada mbalimbali za misitu tangu kuanzishwa kwa taaluma hiyo chuoni hapo na hakikuishia kufundisha pekee kimeendelea kuimarisha mafunzo hayo kwa vitendo ambapo kimetenga Msitu wa Mafunzo Olmotonyi Arusha wenye hekari zipatazo 800, Kitulangalo Morogoro, Msitu wa Mazumbai ambao una hekari 200 pamoja na kupanda msitu mwingine wa mafunzo Ifinga Madaba Songea ambao unatarajiwa kuwa wa hekta elfu 10.
0 Comments