Na: Tatyana Celestine, Winfrida Nicolaus
Imeelezwa
kuwa Ulemavu si kigezo cha kumfanya Mwanafunzi kushindwa
kusonga mbele kielimu na kuyafikia malengo yake kwani jamii inayomzunguka inatakiwa kumjali na kumuongoza katika hatua
stahiki kama wanafunzi wengine.
Kauli
hiyo imetolewa na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Mipango, Utawala na Fedha SUA Prof.
Amandus Muhairwa wakati akifunga mafunzo ya kuwajengea uwezo wanataaluma wa Chuo
hicho juu ya kutambua na kujua namna ya kumuhudumia mtu mwenye mahitaji maalum ili
kuleta usawa kwenye nyanja ya ufundishaji na ujifunzaji.
Prof. Muhairwa
amesema hapo zamani SUA haikuchukua wanafunzi wenye mahitaji maalum lakini sasa
enzi hizo zimekwisha pita hivyo mafunzo hayo yamepanda mbegu ya kutosha kuweza kukiwezesha chuo kwenda mbele katika kutoa
elimu jumuishi bila kujali hali ambazo wanafunzi hao wanakuwa nazo na malengo
yao kuweza kutumia.
Aidha
amesema katika Mradi wa HEET mahitaji maalumu ni moja ya kipaumbele katika kuweka
miundo mbinu ambayo wanaijenga na mingine iliyopo itaboreshwa kwa uwezo wa
kuchukua watu wenye mahitaji maalum Pamoja na kuhakikisha watu hao wanaweza
kujifunza bila tatizo lolote.
“Najua
kama wakufunzi mmefundishwa mbinu za kufundisha watu wenye mahitaji maalum lakini
pis jinsi ya kuwatahini watu hao na
semina kama hii Mradi wa HEET imeupatia uzito mkubwa sana maka kuhakikisha mambo haya yanafika mpaka kwenye
Mitaala ili kuhakikisha mazingira ya kujifunzia yanakuwa salama na rafiki kwa watu
wa aina zote. ”, amesema Prof. Muhairwa
Kwa
upande wake Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Shule Kuu ya Elimu
Idara ya Saikolijia na Mafunzo ya Mitaala Dkt. Lwimiko Sanga amesema mtu mwenye
mahitaji maalum akipewa nafasi ya kufundishwa na kuelekezwa anaweza kufanya
zaidi ya matarajio ja jamii kwakuwa wao pia wanauwezo wa kuajiliwa, ubunifu na
hata kufanya vitu vya aina mbalimbali endapo watapewa nafasi na kuwezeshwa.
Aidha amesema
wanafunzi wenye mahitaji maalum kipindi cha nyuma wamekuwa wakiacha nyuma hasa katika masuala ya elimu kwa kuamini
kuwa watu hao hawana uwezo wa kufanya lolote lakini ukweli ni kwama wana uwezo
wa kufanya vitu mbali mbali kama walivyo wanafunzi wengine kama watapatiwa
mazingira na nyenzo sahihi katika kupata elimu yao.
“Kimsingi walimu au wakufunzi wanaelekezwa namna ambavyo wanaweza kuyatambua haya mahitaji kwasababu wanafunzi wenye mahitaji maalum ni wengi na mahitaji yenyewe ni mengi na kila mahitaji yana namna yake maalum ya kuweza kuyatambua na kuwahudumia hivyo wanataaluma wanapitishwa eneo moja baada ya lingine ili kuweza kujua namna ya kutoa huduma stahiki na huyu mwanafunzi kuweza kunufaika na mafunzo anayoyapata”, amesema Dkt. Sanga
Naye
mmoja wa washiriki katika mafunzo hayo Bw. Anthony Muhando kutoka Idara ya
Upasuaji na Uzalishaji Wanyama
iliyopo Ndaki ya Tiba ya Mifugo
na Sayansi Shirikishi SUA amesema mafunzo
hayo ni msaada mkubwa kwa wakufunzi
ambao wanakutana na wanafunzi mara kwa mara hivyo yatawasaidia kuwatambua watu
wenye mahitaji maalum chuoni na kuboresha namna ya ufundishaji wao kwa lengo la
kuleta usawa.
0 Comments