Katika kufikia malengo ya mwaka 2030 ya kilimo kukua kwa asilimia 10, Wizara ya Kilimo imeingia kwenye makubaliano ya kushirikiana n (SUA) ili kukuza na kuongeza tija ya kilimo kwa wakulima hapa nchini.
Naibu Katibu Mkuu,Wizara ya Kilimo Dkt. Hussein Mohamed Omar akizungumza katika hafla ya kusaini mkataba huo iliyofanyika Jijini Dodoma Desemba 6, 2023, amesema Wizara imeona ni muhimu kushirikiana na taasisi za elimu zinazotoa mafunzo ya kilimo kama sehemu ya mkakati wa kuinua sekta ya kilimo ili ikue sawa na malengo ya Serikali.
Dkt. Omar, amesema kupitia ushirikiano huo wanategemea kuwa wataweza kuwapata wahitimu wengi ambao baadhi yao watakuwa wanapata ajira ya kudumu na wengine kazi za muda kwenda kukut namna bora ya kuzalisha kwa tija.
“Tunafahamu kila mwaka Chuo kama SUA kinazalisha wahitimu wengiambao tunaona tukitumia maarifa na ujuzi walioupata, wakaenda kwenye oa ushauri wakulima wetu wataweza kujua namna ya khivyo uchumi wetu utaweza kukua.”, alisema Dkt. Omar.
Ameongeza kuwa lengo la kushirikiana na taasisi za elimu ni kukuza thamani ya kilimo kwani kilimo kwa miaka mingi kimekuwa uti wa mgongo wa uchumi wa watanzania na kwamba lengo ni kufikia matamani ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kukifanya kilimo kuwa chanzo cha mapato nchini.
Kwa upande wake, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Prof. Raphael Chibunda ameishukuru, akisema ushirikiano huo sasa umekuwa rasmi kwani ulikuwepo kwa muda mrefu.
Prof. Chibunda ameongeza kuwa SUA inaendelea kuwaandaa wanafunzi na hata wasio wanafunzi katika Kituo Atamizi ili baadaye wawe na uwezo wa kulima kilimo biashara.
“Chuo chetu (SUA) tumejipanga kutekeleza makubaliano yaliyopo kwenye huu mkataba lakini tunaweza kweaidi ya haya ambayo tumeyaandika kwenye huu ushirikiano, sisi faraja yetu ni kuona tunakuwa chachu ya kukua kwa kilimo hapa nchini”
Ushirikiano wa Wizara ya Kilimo na SUA ni sehemu ya mikakati ya Serikali ya kuhakikisha kufikia mwaka 2030 kilimo kinakuwa kwa asilimia 10 kutoka nne zilizopo hivi sasa.
0 Comments