Na: Calvin Gwabara – Morogoro.
Wanachama na wadau wa Chama cha Taaluma ya Sayansi ya Kilimo Mazao Tanzania (CROSAT) wanatarajiwa kukutana kwenye mkutano mkuu na Semina maalumu ya Kitaaluma kujadili maendeleo ya sayansi mbalimbali za kilimo nchini.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa
Chama hicho Bwana Patrick Ngwediagi ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya
Uthibiti wa Mbegu Tanzania (TOSCI)wakati akiongea na Waandishi wa habari kuhusu
Mkutano huo na malengo yake kwa wakulima nchini.
“CROSAT ni Chama cha wataalamu wa
kilimo mazao chama hiki ni chama kikongwe lakini mwaka jana Wananchama waliamua
kukiunda upya na kupanga kukutana kwaajili ya kukiendeleza lakini pia kiweze
kuchangia katika maendeleo ya sekta ya kilimo na uchumi nchini” Alisema
Ngwediagi.
Aliongeza” Hivyo kupitia kukutana
kwetu mwaka huu tarehe 19 na 20 mwezi huu wa 12 pale Jijini Dodoma tunalenga siku
ya kwanza kuwa na mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wananchama na siku ya pili tutakuwa
na semina Maalumu itakayotazama na kuhakikisha kunakuwepo na matumizi sahihi na
salama ya viuatilifu na upatikanaji wa mbegu bora kwa wakulima”.
Amesema Duniani na nchini Tanzania
baadhi ya wadau wa kilimo wamekuwa wakitumia viuatilifu ambavyo havistahili au
kutumia isivyo sahihi na matokeo yake ni kuleta hasara kwa wakulima na
kuhatarisha afya na maisha ya watumiaji wa mazao hayo pamoja na wao wenyewe
hivyo mkutano huo utajadili kwa kina na kutoa ushauri wa nini kifanyike katika
kumaliza tatizo hilo.
Amefafanua kuwa tafiti mbalimbali
zimefanyika kuhusu masula ya mifumo ya mbegu pamoja na matumizi ya viuatilifu
hivyo mawasilisho mbalimbali yatafanyika na kujadiliwa kwa kina kwenye siku
hiyo ya pili ya mkutano huo na hivyo kujenga uelewa wa pamoja na kutoka na
maazimio ya namna ya kusaidia wakulima nchini.
Katibu Mkuu huyo wa CROSAT
amesema Kauli Mbiu ya mkutano huo ni “Kujenga kesho iliyo bora kupitia mifumo
bora ya mbegu na matumizi sahihi ya viuatilifu kwaajili ya kilimo endelevu”.
Bwana Ngwediagi amesema mgeni
rasmi kwenye siku ya pili ya Mkutano huo ambayo ndio itafanyika semina hiyo ya
kitaalamu na kuhusisha mawasilisho ya atakuwa na Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein
Bashe.
Kwa upande wake Dkt. Yasinta
Nzogela ambaye ni katibu Msaidizi wa Chama hicho na mdhadhiri kutoka SUA amesema
pamoja na mambo hayo lakini chama kinaendelea kutoa mchango wa kina kwa Wanawake
na vijana ili kusaidia kushiriki kikamilifu kwenye uzalishaji na kuzalisha kwa
tija kwakuwa kundi hilo hasa wanawake ndio washiriki wazuri kwenye kilimo.
“Chama chetu pia kinaendelea
kuhamasisha Wanawake kushiriki vizuri kwa tija kwenye kilimo lakini pia kujiunga
na chama hiki kwakuwa wapo wanawake wengi kwenye taaluma hii serikali, kuu,
serikali za mitaa, mawizarani, mashirikia ya kiserikali na yasiyo ya kiserikali
n ahata baadhi yao wengi wanamakampuni makubwa ya uzaliahaji pia wajiunge na
chama hiki ili tusaidie wengine kuongeza tija” Alisema Dkt. Nzogela.
Nae Makamu Katibu Mwenezi wa chama hicho ambaye pia ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Bi. Jenipher Tairo ametumia nafasi hiyo kuwakaribisha wananchama wote kushirki mkutano huo kwa wingi lakini pia ambao sio wanachama kujiunga mahali popote walipo kwakuwa taarifa zote zipo kwenye tovuti ya Chama ikiwemo form na maelekezo mengine.
Waandishi wa Habari kutoka Vyombo mbalimbali wakifuatilia mkutano huo uliofanyika kwenye ofisi za TOSCI Morogoro. |
Makamu Katibu Mwenezi wa chama hicho ambaye pia ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Bi. Jenipher Tairo akizungumza na Waandishi wa habari. |
Dkt. Yasinta Nzogela ambaye ni katibu Msaidizi wa Chama hicho na mdhadhiri kutoka SUA akifafanua jambo kwa Waandishi wa habari. |
Waandishi wa Habari kutoka Vyombo mbalimbali wakifuatilia mkutano huo uliofanyika kwenye ofisi za TOSCI Morogoro. |
Waandishi wa Habari kutoka Vyombo mbalimbali wakifuatilia mkutano huo uliofanyika kwenye ofisi za TOSCI Morogoro. |
0 Comments