SUAMEDIA

SUA na TPHPA watumia wadudu rafiki kuwakabili Viwavijeshi Vamizi nchini

 Na: Calvin Gwabara - Tanga.

Watafiti wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kwa kushirikiana na watafiti kutoka Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) wanafanya majaribio ya matumzi ya wadudu rafiki kupambana na Viwavijeshi vamizi kwenye mahindi.

Mtafifti Mkuu kutoka SUA Prof.Gratian  Rwegasira na wataalamu kutoka  TPHPA wakiwa kwenye zoezi la kuweka wadudu hao rafiki kwenye mashamba ya wakulima Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro na Muheza mkoani Tanga

Akizungumza na Mwandishi wetu Mkuu wa Mradi huo wa Utafiti Prof. Gration Rwegasira kutoka SUA amesema baada ya utafiti na majaribio ya maabara na baadae ngazi ya kitalu nyumba wamebaini kuwa wadudu aina ya Trichogramma mwanzae na Telenomous remus wameonesha uwezo mkubwa katika kupambana na viwavijeshi vamizi.

‘’Katika utafiti wetu tukabaini wadudu hao aina mbili ambao ni nyigu wadogo sana wenye uwezo wa kuwadhibiti Viwavijeshi vamizi na wao wanauwezo wa kushambulia mayai ya kiwavijeshi na sio kiwavijeshi mwenyewe na hivyo kwakuwa wanashambulia mayai yao wanasababisha kutoongezeka na kupotea kwa viwavijeshi kwa kuwa hawazaliani shambani‘’alieleza Prof. Rwegasira.

Aliongeza ‘’Kwa kuwa tunatambua hatua ambayo inaathiri zaidi mazao ya wakulima ni Kiwavi kwa hiyo mayai yasipoanguliwa maana yake kiwavi hatoanguliwa na hivyo kuwa tumemsaidia mkulima kumaliza wadudu hao hatari kwenye mazao ya mkulima bila kutumia viuatilifu ambavyo vina sumu‘’.

Prof. Rwegasira amesema hivi sasa wapo katika hatua ya tatu ambayo ni kuwapandikiza wadudu hao kwenye mashamba ya wakulima yaliyolimwa Mahindi kwenye Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro na Muheza mkoani Tanga ili kuona namna ambavyo wanafanya kazi kwenye mashamba halisi yenye wadudu aina ya Viwavijeshi Vamizi.

‘’Leo tumeweka kwenye mashamba haya lakini tutarudi kuweka tena baada ya wiki mbili na hii inatakiwa ifanyike mahindi yakishafikisha wiki tatu hadi nne baada ya kupandwa maana majani yatakuwa matatu hadi manne na ndio wakati ambao Viwavijeshi Vamizi wanakuja kutaga mayai yao kwenye mimea kwa hiyo wakifika na kutaga wadudu hao rafiki wanashambulia mayai yote shambani”, alieleza Prof. Rwegasira.

Aidha amesema wadudu hao rafiki wanatumia mayai ya Viwavijeshi Vamizi kuweza kuzaana hivyo ndio maana wanayatafuta mayai hayo na kudunga sindano na kuweka mayai yao ndani ya yai la kiwavijeshi vamizi na kwa namna hiyo wanamaliza kizazi cha Viwavijeshi vamizi kwenye shamba la mkulima na kubaki wao ambao hawana madhara.

Amesema utafiti huu ukikamilika utawasaidia wakulima kuondokana na matumizi ysiyofaa ya viuatilifu vyenye viambata sumu ambavyo ni hatari kwa afya zao na mazingira na zaidi sana hawa wadudu rafiki watampunguzia Mkulima gharama za uzalishaji mazao ya chakula hasa mahindi na kuleta tija kwenye kipato cha kaya na taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake Mkulima Salehe Alfan Ally mkazi wa Dumila Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro amepongeza utafiti huo ambao utasaidia kulinda mazao yao kwa kuwa matumizi ya madawa wengi hawayawezi maana ni ghari na mwisho wa siku wanapata hasara wakati wa kuvuna.

‘’Awali tulizoea kulima mahindi bila kupulizia dawa tukawa tunapulizia dawa kwenye mashamba ya nyanya tu lakini toka mwaka 2017 walipokuja wadudu hawa Viwavijeshi Vamizi hali ya maisha yetu yamekuwa magumu tunapata hasara maana sio wote wanamudu kununua madawa kupulizia kila baada ya wiki mbili hadi tunapovuna na bado hawatoweki‘’ alieleza Bw. Salehe.

 Aliongeza kuwa ‘’Yani inafika mahali tunaamua tu kuacha wadudu wale na kile kinachobaki ndicho tunachopeleka nyumbani kama mavuno ya mwaka na unakuta muda mwingine unapata gunia moja au mbili kwenye shamba la mahindi la ekari moja na unakuta mahindi yenyewe ni yale madogo madogo sana ambayo yameliwa hadi magunzi yamejikunja‘’.

Nae Afisa Kilimo Mwandamizi kutoka Kata ya Mlingano wilayani Muheza mkoani Tanga Bw. Jimmy Mhina amewapongeza watafiti hao wa SUA na TPHPA kwa kuja na ubunifu huo wa matumizi ya wadudu rafiki katika kukabiliana na Viwavijeshi Vamizi na kuomba jitihada hizo za majaribio zifanikiwe kwenye mashamba ili kumtua mkulima mzigo wa hasara zinazosababishwa na wadudu hao hatari kwenye mazao.

‘’Wakulima wengi wanashindwa kununua mfano mbolea na hata mbegu bora sasa ujio wa wadudu hawa unawalazimisha gharama ya kununua Viuatilifu ambavyo ni ghali na hivyo wengi wao hawapigi dawa wanahudumia shamba na kusubiri kile watakachobakisha wadudu hao ndio apeleke kwenye familia kwa kweli wanapata tabu na kuongeza umasikini kwa wakulima wetu‘’ alifafanua bw. Mhina.

Viwavijeshi Vamizi kutoka Amerika viliingia nchini mwaka 2017 kwenye mikoa michache lakini kufikia mwaka 2019 viliripotiwa kwenye mikoa yote ya Tanzania na kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) ambao ndio wafadhili wa utafiti huo wanasema Viwavijeshi Vamizi wanauwezo wa kushambulia mazao zaidi ya 80.Akizungumza na Mwandishi wetu Mkuu wa Mradi huo wa Utafiti Prof. Gration Rwegasira kutoka SUA amesema baada ya utafiti na majaribio ya maabara na baadae ngazi ya kitalu nyumba wamebaini kuwa wadudu aina ya Trichogramma mwanzae na Telenomous remus wameonesha uwezo mkubwa katika kupambana na viwavijeshi vamizi.

‘’Katika utafiti wetu tukabaini wadudu hao aina mbili ambao ni nyigu wadogo sana wenye uwezo wa kuwadhibiti Viwavijeshi vamizi na wao wanauwezo wa kushambulia mayai ya kiwavijeshi na sio kiwavijeshi mwenyewe na hivyo kwakuwa wanashambulia mayai yao wanasababisha kutoongezeka na kupotea kwa viwavijeshi kwa kuwa hawazaliani shambani‘’alieleza Prof. Rwegasira.

Aliongeza ‘’Kwa kuwa tunatambua hatua ambayo inaathiri zaidi mazao ya wakulima ni Kiwavi kwa hiyo mayai yasipoanguliwa maana yake kiwavi hatoanguliwa na hivyo kuwa tumemsaidia mkulima kumaliza wadudu hao hatari kwenye mazao ya mkulima bila kutumia viuatilifu ambavyo vina sumu‘’.

Prof. Rwegasira amesema hivi sasa wapo katika hatua ya tatu ambayo ni kuwapandikiza wadudu hao kwenye mashamba ya wakulima yaliyolimwa Mahindi kwenye Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro na Muheza mkoani Tanga ili kuona namna ambavyo wanafanya kazi kwenye mashamba halisi yenye wadudu aina ya Viwavijeshi Vamizi.

‘’Leo tumeweka kwenye mashamba haya lakini tutarudi kuweka tena baada ya wiki mbili na hii inatakiwa ifanyike mahindi yakishafikisha wiki tatu hadi nne baada ya kupandwa maana majani yatakuwa matatu hadi manne na ndio wakati ambao Viwavijeshi Vamizi wanakuja kutaga mayai yao kwenye mimea kwa hiyo wakifika na kutaga wadudu hao rafiki wanashambulia mayai yote shambani”, alieleza Prof. Rwegasira.

Aidha amesema wadudu hao rafiki wanatumia mayai ya Viwavijeshi Vamizi kuweza kuzaana hivyo ndio maana wanayatafuta mayai hayo na kudunga sindano na kuweka mayai yao ndani ya yai la kiwavijeshi vamizi na kwa namna hiyo wanamaliza kizazi cha Viwavijeshi vamizi kwenye shamba la mkulima na kubaki wao ambao hawana madhara.

Amesema utafiti huu ukikamilika utawasaidia wakulima kuondokana na matumizi ysiyofaa ya viuatilifu vyenye viambata sumu ambavyo ni hatari kwa afya zao na mazingira na zaidi sana hawa wadudu rafiki watampunguzia Mkulima gharama za uzalishaji mazao ya chakula hasa mahindi na kuleta tija kwenye kipato cha kaya na taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake Mkulima Salehe Alfan Ally mkazi wa Dumila Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro amepongeza utafiti huo ambao utasaidia kulinda mazao yao kwa kuwa matumizi ya madawa wengi hawayawezi maana ni ghari na mwisho wa siku wanapata hasara wakati wa kuvuna.

‘’Awali tulizoea kulima mahindi bila kupulizia dawa tukawa tunapulizia dawa kwenye mashamba ya nyanya tu lakini toka mwaka 2017 walipokuja wadudu hawa Viwavijeshi Vamizi hali ya maisha yetu yamekuwa magumu tunapata hasara maana sio wote wanamudu kununua madawa kupulizia kila baada ya wiki mbili hadi tunapovuna na bado hawatoweki‘’ alieleza Bw. Salehe.

 Aliongeza kuwa ‘’Yani inafika mahali tunaamua tu kuacha wadudu wale na kile kinachobaki ndicho tunachopeleka nyumbani kama mavuno ya mwaka na unakuta muda mwingine unapata gunia moja au mbili kwenye shamba la mahindi la ekari moja na unakuta mahindi yenyewe ni yale madogo madogo sana ambayo yameliwa hadi magunzi yamejikunja‘’.

Nae Afisa Kilimo Mwandamizi kutoka Kata ya Mlingano wilayani Muheza mkoani Tanga Bw. Jimmy Mhina amewapongeza watafiti hao wa SUA na TPHPA kwa kuja na ubunifu huo wa matumizi ya wadudu rafiki katika kukabiliana na Viwavijeshi Vamizi na kuomba jitihada hizo za majaribio zifanikiwe kwenye mashamba ili kumtua mkulima mzigo wa hasara zinazosababishwa na wadudu hao hatari kwenye mazao.

‘’Wakulima wengi wanashindwa kununua mfano mbolea na hata mbegu bora sasa ujio wa wadudu hawa unawalazimisha gharama ya kununua Viuatilifu ambavyo ni ghali na hivyo wengi wao hawapigi dawa wanahudumia shamba na kusubiri kile watakachobakisha wadudu hao ndio apeleke kwenye familia kwa kweli wanapata tabu na kuongeza umasikini kwa wakulima wetu‘’ alifafanua bw. Mhina.

Viwavijeshi Vamizi kutoka Amerika viliingia nchini mwaka 2017 kwenye mikoa michache lakini kufikia mwaka 2019 viliripotiwa kwenye mikoa yote ya Tanzania na kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) ambao ndio wafadhili wa utafiti huo wanasema Viwavijeshi Vamizi wanauwezo wa kushambulia mazao zaidi ya 80.

Mdudu rafiki aina ya Telenomus remus,akitoboa na kutaga mayai yake kwenye mayai ya Kiwavijeshi Vamizi.

Mdudu rafiki aina ya Trichogramma mwanzae akitoboa na kutaga mayai yake kwenye mayai ya Kiwavijeshi Vamizi.

Mtafifti Mkuu kutoka SUA Prof.Gratian  Rwegasira na wataalamu kutoka  TPHPA wakiwa kwenye zoezi la kuweka wadudu hao rafiki kwenye mashamba ya wakulima.

Picha ya karibu ya namna Kiwavijeshi vamzi anavyoshambulia zao la Mahindi.

Sehemu ya mashamba ya Mahindi ya wakulima Wilayani Mvomero yaliyoathiriwa na Viwavijeshi Vamizi.

Sehemu ya picha anayoonesha wadudu hao rafiki wakiwa kwenye maabara kwenye Maabara za TPHPA kibaha.

Post a Comment

0 Comments