SUAMEDIA

SUA yapongezwa kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo

NA Winfrida Nicolaus

Menejimenti ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA imepongezwa kwa hatua nzuri ambayo wameifikia katika Ukarabati na Ujenzi wa majengo kupitia Miradi mbalimbali Chuoni hapo na kutakiwa kuhakikisha wanaendelea kuisimamia vizuri miradi hiyo ili ikamilike kwa wakati.

Pongezi hizo zimetolewa na Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Bi. Dorothy Mwanyika ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha, Mipango na Maendeleo kwenye Ziara ya Kamati ya Fedha, Mipango na Maendeleo kwenye maeneo ya SUA yaliyopo kwenye ukarabati ikiwemo Mradi wa ukarabati wa Hosteli ya ICE, Ujenzi wa  Jengo la Mradi wa ACE II-IRPM na BTD, mradi wa ukarabati wa majengo ya Kihonda Magorofani pamoja na ukarabati wa Jengo la Hostel za X-NBC

Amesema katika kuangalia kiwango cha kazi kimeonesha kuwa kazi imefanyika vizuri, thamani ya Fedha imeonekana, wasimamizi wamesimamia kazi vizuri vilevile hata changamoto ambazo zimekuwa zikijitokeza zimeshughulikiwa kwa wakati hivyo kupelekea Miradi yote iliyopo kwenye ukarabati ambayo wameitembelea imefikia mahali pazuri na wanatumaini kuwa itakamilika kwa wakati uliopangwa.

Bi. Dorothy amesema kupitia Ziara hiyo wameona ni jinsi gani SUA ina mali nyingi ambazo zinaweza kugeuzwa kuwa fursa za kiuchumi hivyo wanatarajia baada ya tu ya ziara kutakuwa na ubunifu zaidi kwa kuangalia namna Rasilimali za Kiuchumi ambazo wanazo kuzigeuza kuwa vyanzo vya mapato.

“Ilikuwa katika kikao chetu cha Kamati ya Fedha, Mipango na Maendeleo kilichofanyika Juni 12, 2023 kama kamati tuliona kwamba ni vizuri tutembelee Miradi ambayo inatekelezwa na Menejimenti ya SUA hivyo tunaishukuru Menejimenti imezingatia ushauri na kuandaa ziara hiyo”, amesema Bi Dorothy Mwanyika.












Post a Comment

0 Comments