SUAMEDIA

Maonesho ya TCU yafungwa, SUA yajivunia mafanikio

 Na: Farida Mkongwe

Maonesho ya Vyuo Vikuu yaliyokuwa yakifanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar Es Salaam yamehitimishwa rasmi ambapo Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kimesema kimefanikiwa kufanya usajili wa zaidi ya wanafunzi 6,000 ambao wameomba kujiunga na Chuo hicho.



Mhadhiri na Mkuu wa Kitengo cha Elimu ya Kujiendeleza na Ugani Dkt. Emanuel Malisa akipokea cheti cha ushiriki kutoka kwa N
aibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omary Kipanga.Picha na Asifiwe Mbembela.

Akizungumza baada ya kufungwa Maonesho hayo Mhadhiri na Mkuu wa Kitengo cha Elimu ya Kujiendeleza na Ugani Dkt. Emanuel Malisa amesema pamoja na kusajili wanafunzi hao pia wamefanikiwa kutoa elimu kwa wananchi kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na SUA sambamba na kutengeneza mawasiliano ya namna ya kuwafikia wataalamu wa SUA pindi mwananchi atakapokuwa na uhitaji wa bidhaa mbalimbali.

Katika hafla hiyo ya ufungaji Chuo Kikuu cha Sokoine kilikuwa ni miongoni mwa Vyuo vilivyopokea Cheti cha Ushiriki kilichotolewa na Mgeni Rasmi ambaye alikuwa ni Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omary Kipanga (Mb) ambapo Dkt. Malisa amesema cheti hicho ni heshima kubwa sana kwa Chuo hicho.

“Hiki ni Cheti cha Ushiriki ambacho kimetolewa na TCU kwetu sisi ni ishara ya heshima kubwa kwamba TCU wamethamini ushiriki wetu na ni chachu kwa ajili ya kufanya vizuri zaidi, kiukweli hakuna shaka  Chuo chetu kinafanya vizuri na hata ukiangalia watu wanaopita hapa maoni wanayotoa ni ya kuridhisha “, amesema Dkt. Malisa.

Akizungumzia mafaniko ya Chuo hicho Afisa Mahusiano na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko SUA Bi. Suzana Magobeko amesema SUA ni Chuo bora kabisa na Kikongwe nchini Tanzania na Ukanda wa Afrika Mashariki.

“Niwatake wadau na wananchi wote kufika Chuoni kwetu kujipatia Elimu kuhusu masuala ya Kilimo na Mifugo. Pia kwa wale wahitimu ambao hawakuweza kutufikia katika Maonesho ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia wanaweza kupata taarifa zaidi kwa kutembelea tovuti yetu  www.sua.ac.tz  na ili kujisajili ingia 

http://197.250.34.38:8389/index.php/registration 


Post a Comment

0 Comments