NA:Winfrida Nicolaus
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kimepongezwa kwa kutunza, kulinda na kuhifadhi maeneo ya kihistoria ambayo yalitumika wakati wa harakati za ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika ili historia hiyo isipotee na iweze kutumika kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
Pongezi hizo zimetolewa na Brigedia Jenerali AP Charo Mwenyekiti wa Kamati iliyoundwa na Mkuu wa Majeshi nchini Tanzania kwa ajili ya kupitia maeneo mbalimbali ambayo walipita wapigania Uhuru wa nchi za Kusini mwa Afrika wakati alipotembelea Kampasi ya Solomon Mahlangu tarehe 14 Aprili, 2023 kwa ajili ya kujionea utunzaji wa Eneo la Kihistoria la wapigania Ukombozi wa Afrika Kusini.
Amesema SUA kama sehemu inayotunza maeneo ya historia ya ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika imeweza kuweka kumbukumbu zote vizuri ukilinganisha na baadhi ya maeneo mengine ya kihitoria nchini hivyo amejisikia fahari kutembelea Solomon Mahlangu moja ya eneo kati ya maeneo ya kihistoria ambayo lengo kubwa ni kuweza kutangazwa katika Urithi wa Taifa.
“Niwapongeze sana SUA kwa kuendelea kutumia na kuhifadhi maeneo haya, tumeona pamoja na kwamba yalitumika katika harakati za ukombozi, lakini kimsingi miundombinu mikubwa iliyoachwa inaendelea kuhifadhiwa vizuri ili kuhakikisha historia hii haipotei na hii ina manufaa makubwa kwa Taifa letu” alisema Brigedia Jenerali AP Charo
Kwa upande wake Prof. Allen Malisa Rasi Mstaafu Ndaki ya Sayansi na Elimu Kampasi ya Solomon Mahlangu amesema wanajivunia kuwa sehemu ya maeneo yanayotunza historia za Ukombozi wa Nchi za Kusini mwa Afrika tangu walipokabidhiwa rasmi eneo hilo mwaka 1992 hivyo wanachokifanya ni huhakikisah eneo hilo linalindwa na kutunza vyema kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo
Vilevile Eneo hilo la kihistoria limekuwa na manufaa makubwa kwao kwa kuwa linatumika kwa ajili ya kutolea mafunzo zaidi katika kuongeza Udahili lakini pia wao kama SUA wanajivunia kutunza mahusiano baina ya nchi kupitia wageni wanaokwenda kutembelea eneo hilo toka sehemu mbali mbali ndani na nje ya Tanzania.
Katika Picha.
Picha na Tatyana Celestine.
Katika video Bofya hapa chini
chinihttps://youtu.be/2JJKW-mqaA4
0 Comments