Na: Gerald Lwomile, Dodoma
Maonesho ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu kwa
mwaka 2023 yameanza rasmi Aprili 24, 2023 Jiji Dodoma na Chuo Kikuu cha Sokoine
cha Kilimo (SUA) ni miongoni mwa washiriki wa maonesho hayo.
Wananchi mbalimbali waliotembelea banda la SUA wakipata maelezo ya dawa mbalimbali zitokanazo na mimea zilizotengezwa na watafiti kutoka SUA (Picha zote na Gerald Lwomile) |
Kutokana na ushiriki huo SUA imesema teknolojia na bunifu
mbalimbali zinazoibuliwa na wanafunzi na watafiti zinalenga kuhakikisha zinaisaidia
jamii ya kitanzania katika kukabiliana na changamoto mbalimbali.
Hayo yamesemwa leo Aprili 25, 2023 na Profesa Mshiriki Abdul
Katakweba wakati akizungumza na SUAMEDIA Jijini Dodoma kwenye maonesho ya
Ubunifu Kitaifa yanayofanyika jijini hapo.
Profesa Katakweba amesema katika Banda lao lililopo katika
uwanja wa maonesho wa Jamhuri kuwa SUA imekuja na teknolojia mbalimbali ambazo
zinautatuzi kuanzia kwa binadamu, mimea na mifugo.
Maonesho hayo ambayo yanawashirikisha wabunifu kutoka Taasisi
na wadau mbalimbali nchini yameanza rasmi leo Aprili 25, 2023 na yanatarajiwa
kumalizika tarehe 28 Aprili, 2023.
0 Comments