Na: Winfrida Nicolaus
Makamu wa Mkuu wa Chuo cha Sokoine
cha Kilimo (SUA) Prof. Raphael Chibunda amewataka washiriki wa Mafunzo ya
Kujenga Uwezo wa Kuandaa na Kuboresha Mitaala ya SUA kuyatumia mafunzo hayo
kupata uelewa na kwenda kuandaa Mitaala itakayokidhi na kuzingatia mahitaji ya soko
la ajira.
Makamu wa Mkuu wa Chuo cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Prof. Raphael Chibunda akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo (Picha zote na Ayoub Mwigune) |
Amebainisha hayo wakati wa ufunguzi
wa mafunzo hayo kwa siku ya pili ambayo ni sehemu ya Mradi wa Elimu ya Juu kwa
Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) yaliyofanyika katika ukumbi wa Mabara Mtambuka
Kampasi ya Edward Moringe mkoani Morogoro Aprili 25, 2023.
Prof. Chibunda amesema SUA pamoja na
mambo mengine inahitaji kuboresha Mitaala yake ili kuendelea kutoa mafunzo
yanayolenga kumjengea mwanafunzi ujuzi, weledi na stadi za kujiajiri na
kuajirika.
Amesema ili kufikia lengo hilo SUA inahitaji
mitaala inayojumuisha maarifa ya kisasa yanayolingana na mahitaji ya soko la
ajira inayotilia mkazo umahiri, kukuza stadi za kazi na inayozingatia viwango
vya kimataifa.
Kwa upande wake mmoja wa wawezeshaji wa mafunzo hayo Ofisa Mwandamizi wa Elimu ya Juu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia na Mratibu Msaidizi wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya kiuchumi (HEET) ambaye ni Afisa Mwandamizi wa Elimu ya Juu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia na Mratibu Msaidizi wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya kiuchumi (HEET) Dkt. Evaristo Mtitu amesema kati ya mambo manne ambayo Mradi wa HEET unataka kutekeleza moja wapo ni uhuishaji na uandaaji wa Mitaala.
Amesema wanataka kuanzisha Mitaala
isiyopungua 300 na kuboresha iliyopo ili ikidhi mahitaji ya sasa na baadae ya
Taifa na itakayowawezesha wanafunzi kupata Maarifa au Stadi za kuajirika hivyo
mafunzo haya kimsingi yataenda kuwajenea uwezo wanataaluma wa SUA katika
kuhakikisha kuwa Mitaala iyoboresha inakuwa na sifa ya kumuwezesha mwanafunzi
kupata ujuzi stahiki.
"Mwanzoni Mitaala ilielekeza
zaidi kwenye kukuza fikra za wanafunzi lakini sio kuwawezesha kupata stadi za
kuwafanya kuwa wabunifu, watafutaji au watengeneza ajira na badala yake Mitaala iliwaandaa kutegemea ajira za serikali hivyo naamini kupitia mafunzo haya
wanataaluma wa SUA wataenda kwenye idara zao na kuanza kuandaa Mitaala
itakayokidhi vigezo", amesema Dkt. Mtitu
0 Comments