Na: Amina Hezron, Mbeya
Ili
kuhakikisha mazingira ya mto Mbarali na Vyanzo vyake vinatunzwa Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali mkoni Mbeya Mwl. Missana Kwangura ameahidi
kuwajengea mfumo wa maji wanajumuiya ya watumia maji wa
Mto Mbarali (JUWAMBA) ili kurahisisha utunzaji wa kitalu cha miche rafiki
wa maji.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali mkoni Mbeya Mwl. Missana Kwangura (Kulia) akizungumza Mtafiti Mkuu wa Mradi wa (EFLOWS) Prof. Japhet Kashaigili alipotembelea kialu hicho cha miti rafiki na maji kwenye na Wanajumuiya ya watumia maji wa Mto Mbarali (JUWAMBA).
Ahadi
hiyo ameitoa alipokwenda kutembelea sehemu kilipoanzishwa kitalu hicho kupitia
Mradi wa Tathimini ya Maji kwa Mazingira (EFLOWS) akiwa ameambatana na kiongozi
wa mradi huo Prof. Japheti Kashaigili kutoka SUA na kukutana na wanajumuiya hao
ambao ndio wanaotunza kitalu hicho.
Amesema
kuwa kabla mradi huo haujaisha Halmashauri kwa kushirikiana na wenye mradi
pamoja na Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) watajitahidi kuhakikisha mfumo wa
maji umeshakamilika ili kuwatua wakina mama waliopo kwenye jumuiya hiyo ndoo
kichwani kwakuwa wanafanya shughuri hiyo ya umwagiliaji kwakuchota maji mtoni
na kubeba kichwani.
“Tukiweka
mfumo wa maji hapa itasaidia kuoteshwa kwa miche mingi zaidi kutokana na urahisi
wa upatikanaji wa maji jambo litakalokwenda kusaidia kupatikana kwa kipato kwa
Wanajumuiya hawa ambao wanafanya kazi kwa kujitolea endapo watatumia kitalu
hiki kuzalisha na miche ya matunda mwaka mzima ”, alisema Mwl Mwal Kwangura .
Aidha
Mwl Kwangura ameshukuru Watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA)
na Baraza la Usimamizi na Uhifadhi wa Mazingira (NEMC) kwakuanzisha kitalu
hicho cha miti kwakuwa jitihada hizo zinawasaidia sana katika kuungana na
malengo ya Serikali ya kuhakikisha kila halmashauri inapanda miti milioni 1.5
kwa mwaka.
Kwa upande wake mkuu wa mradi wa Tathimini ya
Maji kwa Mazingira (EFLOWS)
Prof.
Japhet Kashaigili ameishukuru halmashauri kupitia Mkurugenzi kwa nia yake ya
kuhakikisha uendelevu wa mradi huo hasa upandaji wa miti kwenye mito na vyanzo
vya maji kwa kutunza kitalu hicho ili kupata miche kupitia wanajumuiya hao
ambao wamejengewa uwezo.
“Tulikuwa tunajiuliza tunaondoka tutaondokaje na
sisi mioyo yetu ingetuuma sana unapoanzisha kitu kama hiki kwa pesa nyingi
halafu siku moja unatembea huku unakuta kimekufa, mimi nishukuru sana kwakuwa
tunaona taa nzuri na mwanga wa
tunakoelekea tunaamini kuwa kazi hii tuliyoianzisha sasa unakuwa endelevu kwa
maslahi mapana ya Wilaya na Taifa.
Aidha Prof. Kashaigili amewataka Wanajumuiya
kufanya kazi hiyo kwa bidii kwakuwa tayari wameshapata watu watakaoshirikiana
nao katika shughuri hiyo ya utunzaji wa kitalu pindi mradi utakapomalizika na
kuahidi kuwapeleka Wanajumuiya wote SUA kupata mafunzo kuhusu uzalishaji wa
miche ya matunda ili kuwaongezea kipato kupitia kitalu hicho na kuendelea
kutunza mazingira na vyanzi vya maji.
Mradi
huu unatekelezwa na Chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kwa kushirikiana na
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa mazingira na unatekelezwa katika
dakio la mto Mbarali katika bonde la mto Rufiji kwa ushirikino na Bodi ya Maji
ya mto Rufiji, Jumuiya za watumia maji, TFS, Wilaya ya Mbarali na Wanging’ombe
na jamii, kwa ufadhili wa Programu ya Mazingira ya Umoja wa Mataifa (UNEP) na
kutelezwa kupitia Sekretarieiti ya Azimio la Nairobi.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali mkoni Mbeya Mwl. Missana Kwangura akipanda mti rafiki wa maji nje ya Kitalu hicho kama alama ya ushiriki wa halmashauri yake katika kuendeleza kitalu hicho. |
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali
mkoani Mbeya Mwl. Missana Kwangura (Kushoto) akizungumza na Mwenyekiti wa (JUWAMBA) bwana Siasa juu ya ujenzi wa mfumo wa
maji na uendelezaji wa kitalu hicho. |
0 Comments