SUAMEDIA

Wafanyakazi watakiwa kuzingatia miiko na maadili ya kazi

NA; AYOUB MWIGUNE

Wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) na nchini kwa ujumla wametakiwa kuzingatia miiko na maadili ya kazi katika utendaji kazi wao ili waweze kufanikisha malengo na mikakati ya Chuo hicho.

Hayo yamezungumzwa  Machi 21, 2023 na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Fedha, Utawala na  SUA Prof. Amandus Mhairwa wakati wa kuhitimisha   mafunzo ya Uthibiti wa Maadili na Kudhibiti Rushwa yaliyotolewa kwa watumishi wapya walioajiriwa hivi karibu na wale waliohamia katika Chuo hicho.

“Mategemeo yetu ni makubwa sana na tunatarajia watatumia nafasi hii ya leo kujifunza na kuanza kuyafanya majukumu yao kinachotegemewa kuanzia sasa ni utumishi wao utakuwa uliotukuka zaidi kuliko kama wangekuwa hwajapata mafunzo haya ” amesema Prof. Mhairwa.

Aidha Prof. Mhairwa amewataka wafanyakazi wa Chuo hicho kutimiza wajibu wao kuheshimu maadili  ya kazi ambapo kwa kufanya hivyo shughuli za kitaaluma zitainuka huku akiwa na matumaini makubwa na waajiriwa hao ambao wengine wao wamepita katika Taasisi nzuri za Elimu zinazoeleweka.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kuthibiti Uadilifu (KKU) SUA Prof. Christopher Mahonge amesema  kamati hiyo imekuwa ikitekeleza majukumu mbalimbali kama kujenga uwezo na kuongeza uelewa juu ya uadilifu na ndio maana wameandaa mafunzo hayo kwa waajiriwa hao ili kutekeza majukumu yake .

“Kuwepo kwa Kamati  hii kunasaidia kuwafanya wafanyakazi wazingatie miongozo ya kimaadili katika ufundishaji wao na ndio maana si swala la kupokea tu malalamiko kutoka kwa wadau lakini pia swala la kujenga uwezo au kuongeza ualewa kuhusu  masuala ya uadilifu na ndio maana  siku ya leo tumekuwa na mafunzo” amesema Prof.Mahonge. 

Kwa upande wa washiriki katika mafunzo hayo  Anastazia Bikuba ambaye ni Mkufunzi Msaidizi  pamoja na Mbonea Mweta ambaye ni mfanyakazi Mwanataaluma kutoka Ndaki ya Misitu Wanyamapori na Utalii wameishukuru menejimenti ya SUA kupitia Kamati ya Kuthibiti Uadilifu (KKU) SUA  kwa mafunzo hayo na kusema kuwa wao kama waajiriwa wapya wataweza kuishi kwa kutimiza wajibu wao kwa kuzingatia maadili ya Umma.

“Semina hiii imetatoa mwanga wa namna bora wa kuweza kutimiza majukumu yetu na kama tutaweza kuishi miongozo tuliyopata lbasi tutaweza kuboresha utendaji kazi wetu na yale malengo ya Taasisi yetu ikiwemo tafiti,mafunzo pamoja na shughuli za ugani zitaweza kutimizwa,” amesema Bw. Mweta


 

 





 

Post a Comment

0 Comments