SUAMEDIA

Mradi wa Ujenzi wa Vyuo Vikuu Imara (BSU) chachu ya kuinua taaluma SUA

Na: Tatyana Celestine

Nafasi za kujiendeleza kielimu kwa Wanataaluma katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kupitia Mradi wa Ujenzi wa Vyuo Vikuu Imara (BSU) ushirikiano kati ya watafiti wa SUA na Serikali ya  Denmark kupitia Vyuo Vikuu mbalimbali wakiunganishwa na Shirika la Misaada la Denmark (DANIDA) zimekuwa chachu ya kuinua taaluma chuoni hapo kutokana na matokeo ya elimu hiyo kwa Chuo.




Akizungumza mara baada yakufunga mradi huo Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Prof. Raphael Chibunda amesema kuwa elimu katika makundi tofauti ya wanataaluma waliopata kupitia mradi huo imepelekea Chuo kunufaika katika nyanja tofauti hasa kwa upande wa Kilimo Mseto SUA, kuongeza Shahada ya Uzamivu ambapo kwa sasa wanafunzi wanaendelea na masomo yao kikamilifu.

Aidha Prof. Chibunda amewataka vijana wanaojituma kutoka SUA ambao wamepata elimu kutoka BSU na kupelekea kuibua vijana wengine ambao watakuwa faida kwa chuo kama alivyofanya kijana muhitimu wa SUA ambaye ameweza kutengeneza program yenye uwezo wa kutumika na wafugaji hasa wa samaki pindi wanapokuwa na matatizo ili kuwasiliana na wataalamu.

“Huyu kijana ni sehemu ya vijana wetu ambao wametembea kwenye maono ya Chuo… wanafunzi wanaosoma Chuo hiki lengo letu sio kuwafanya wamalize na wapate vyeti ili waende kutafuta kazi lakini ni kuwapa ujuzi na weledi vilevile kuwapa uthubutu anapoweza kutumia maarifa yake akayafanyia biashara”, amesema Prof. Chibunda.

Aidha amewaasa wanachuo waliomaliza masomo yao kupitia SUA wawatumie wanachuo wenzao waliofanikiwa ili kujifunza kwani kukaa chuoni kwa zaidi ya miaka mitatu kuna uwezekano wa kutumia walichokipata na kuwaletea tija katika safari yao kielimu na kujitegemea katika maisha yao.

Mradi wa Ujenzi wa Vyuo Vikuu Imara (BSU), uliendeshwa kwa awamu tatu ndani ya miaka 10 mpaka kuhitimishwa kwake March 22, 2023 na uliweza kushirikisha Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA), Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (KCMC)  na Serikali ya  Dermark kupitia Vyuo vyake mbalimbali pamoja na wadau wengine nchini.









Post a Comment

0 Comments