Na: Tatyana Celestine
Kutokana na ustawi na mafanikio kwa vijana wengi nchini kupitia Kituo Atamizi kilichopo Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Vijana nchini wametakiwa kutoacha kutumia nafasi ya mafunzo yatolewayo chuoni hapo ili kuondokana na dhana ya kuwa ajira hakuna na hivyo kufanya vijana wengi kushindwa kujipatia kipato cha kukidhi mahitaji ya maisha yao.
Kamati ya Wakaguzi ilitembelea Kituo Atamizi SUA na kujionea mafanikio ya vijana kupitia kituo hicho. |
Hayo yamesemwa na Kamishna Msaidizi wa Bajeti ya Serikali Wizara ya Fedha na Mipango ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ukaguzi SUA Bi. Bahati Mgongorwa wakati akizungumza na SUAMEDIA mara baada ya Ziara ya kutembelea katika Kituo Atamizi kilichopo SUA pamoja na Hospitali ya Taifa ya Rufaa ya Wanyama iliyopo chuoni hapo.
“Eneo ambalo linaitwa Kituo Atamizi nilichojifunza na cha kufanyia kazi ni fursa ambazo zinatolewa kwa vijana wetu kwa sababu vijana wanaoingia pale hawachagui ukiwa Darasa la Saba unaweza kujiunga ,Kidato cha Nne na Chuo Kikuu unaweza kujiunga na Kituo hicho”, amesema Bahati Mgongorwa.
Nae Kaimu Mkurugenzi wa Mafunzo Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi Bw. Amani Ngonyani amesema kuwa mbali na mafanikio yote kwa vijana wanayopata kupitia Kituo Atamizi SUA wanatakiwa waweze kupatiwa elimu ya kutafuta masoko ya bidhaa wanazozalisha ili waweze kupata faida kubwa itakayowapelekea kufikia ndoto zao kama vijana.
“Kwa mfano kijana David ameonesha kuwa na wasiwasi kwa sababu mara zote kunakuwa na mawakala na hao wanapata faida zaidi ya mzalishaji….kama SUA inaweza ikatengeneza program ambayo itasaidia vijana kuweza kufikia wenyewe masoko hayo itawasaidia sana hususani vijana kama akina David,” amesema Bw. Ngonyani.
Kaimu Mkurugenzi wa Mafunzo Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi Bw. Amani Ngonyani (wa kwanza kushoto) akiangalia mazao yaliyozalishwa na vijana wa Kituo Atamizi SUA. |
0 Comments