SUAMEDIA

SUA Kampasi ya Mafunzo Olmotonyi kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali

Na: Tatyana Celestine  

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Kampasi ya Mafunzo Olmotonyi kimeendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika suala la utunzaji wa mazingira ili kuepukana na athari zinazoletwa na mabadiliko ya tabia nchi kwa jamii.


Picha  kutoka Maktaba

Kaimu Meneja wa Kampasi  ya Olmontonyi Bw. Said Kiparu amesema  Chuo kimeendelea na utunzaji mzuri wa mazingira lengo likiwa ni kuhuisha mazao yatokanayo na misitu tangu kuanzishwa kwake mnamo mwaka 1978 ikiwa ni Hifadhi ya Msitu wenye  hekta 865.

Kaimu Meneja huyo amebainisha kuwa mbali na Chuo kutoa mafunzo kwa vitendo kwa Ngazi za Shahada za Misitu kwa wanafunzi lakini pia Chuo kinaungana na wananchi waishio karibu na msitu huo katika kuandaa mashamba, kulima na kupanda mazao ya muda mfupi.

Aidha Bw. ameshukuru kuletwa wa Mashine ya slide Tec Sawmill 2020 yenye uwezo wa kuchakata magogo asilimia 48-50 wakati hapo awali zilitumika mashine nyingine zilizochakata mbao kwa asilimia 33-40 hali ambayo ni mafanikio kwao.

Pamoja na mambo mengine Bw. Kiparu amewahakikishia wananchi kuwa Kampasi ya Olmontonyi ni Kituo Bora kwaajili ya mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi hivyo matarajio ya Chuo kwa sasa ni kuongeza uzalishaji wa mazao ya Misitu kwa kutumia Teknolojia mpya, kusaidia kuendesha kituo ikiwemo kupunguza gharama za uendeshaji pamoja na kukuza pato la Serikali ambapo Chuo kitatoa asilimia 18.




Post a Comment

0 Comments