Na,
Gerald
Lwomile
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo
(SUA) kimesema hakitawavumilia watumishi wote wanaoenda kinyume na Sheria,
Kanuni na Taratibu zilizoainishwa kwa watumishi wa Serikali.
Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Raphael Chibunda akizungumza na watumishi wa SUA hawapo pichani wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo (Picha zote na Ayoub Mwigune)
Akizungumza Machi 21, 2023 katika ufunguzi wa mafunzo ya Uthibiti wa Maadili na Kudhibiti Rushwa yanayotolewa kwa watumishi wa SUA walioajiriwa hivi karibu na wale waliohamia katika Chuo hicho, Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Raphael Chibunda amesema kinayachulia mafunzo hayo kwa umuhimu mkubwa kwani ni kutekeleza agizo la Serikali Kuu.
Prof. Chibunda amesema SUA
itawachukulia hatua kali kwa mujibu wa kanuni na sheria za utumishi wa umma
watumishi wote ambao watakiuka kwa makusudi na hata kwa uzembe katika utekelezaji
wa majumu yao.
“Sisi kama Chuo Kikuu cha Sokoine
cha Kilimo tunatilia maanani na umuhimu wa pekee kwa wafanyakazi wetu kuweza
kufahamu taratibu zote ambazo zinatelekezwa na sheria mbali za Serikali kuhusu
uadilifu katika utumishi wa umma na kupiga vita rushwa katika Taasisi yetu na Serikali
kwa ujumla” amesema Prof. Chibunda
Wafanyakazi wa SUA pichani wakifuatilia mafunzo kutoka kwa wawezeshaji
Awali akizungumza kabla ya Mgeni
Rasmi Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo upande wa Taaluma,
Utafiti na Ushauri wa Kitaalam Prof. Maulid Mwatawala amewataka watumishi hao
kuhakikisha wanaujua utamaduni wa Taasisi wanayoifanyia kazi yaani SUA.
Amesema watumishi wengi wamekuwa
hawajui tamaduni ya Taasisi jambo ambalo limekuwa likileta mchanganyiko katika
utendaji wa kazi, aidha amewataka watumishi hao kuacha tamaa katika maeneo yao
ikiwa ni pamoja na kuepuka rushwa.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya
Kuthibiti Uadilifu (KKU) SUA Prof. Christopher Mahonge amesema uongozi wa juu wa
Taasisi hiyo umekuwa ukiunga mkono jitihada za Kamati hiyo jambo linaloweza
kuzaa matunda mazuri ya kuwa na watumishi wenye uadilifu na wasiopokea rushwa.
0 Comments