Na Gerald Lwomile
Watafiti katika Chuo Kikuu
cha Sokoine cha Kilimo (SUA) wametakiwa kufahamu kuwa pamoja na kufanya tafiti
ambazo zitachapishwa kwenye machapisho ya kisayansi, lakini ni muhimu tafiti
zao zikazigusa jamii na kuziletea mabadiliko chanya.
Prof. Esron Karimuribo akizungumza katika ufunguzi wa warsha ya kuwajengea uwezo watafiti SUA (Picha zote na Gerald Lwomile)
Rai hiyo imetolewa Machi 29,
2023 na Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Boniface Mbilinyi katika hotuba
yake iliyosomwa na Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu
cha Sokoine Cha Kilimo Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalam ambaye ni
Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Uzamili, Utafiti, Uhaulishaji wa
Teknolojia na Ushauri wa Kitaalam Prof. Esron Karimuribo wakati akifungua warsha ya kuwajengea uwezo watafiti wa namna ya uandishi
wa madodoso ya kitafiti na usimamizi wa miradi ya kitafiti.
Prof. Karimuribo amesema
jamii ya kitanzania na hasa watu waishio vijiji, kata na wilaya watakazokwenda kufanya
utafiti wajisikie na kuona kuwa SUA inawatendea haki na hasa katika kuhakikisha
wanapata maendeleo kupitia miradi hiyo ya kitafiti.
Aidha amesema kuwa
watafiti hao ambao ni wanufaika wa mafunzo hayo,
wanatakiwa kuona fahari na bahati ya kipekee kwani kuna baadhi ya watafiti
hawakufikia matarajio yao.
Amewataka watafiti hao
kuzingatia kutoa matokeo ya utafiti bora wa kisayansi na hata ukichapishwa
uweze kuakisi dhamira ya SUA kwani Chuo hicho kimekuwa kikishika nafasi ya kwanza
katika nafasi ya Vyuo Vikuu vilivyo na tafiti bora zaidi nchini Tanzania
Akitoa shukrani kwa Mgeni
rasmi ambae ni Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha
Sokoine cha Kilimo Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalam, Mratibu wa
Teknolojia na Ushauri wa Kitaalam SUA Dkt. Doreen Ndosi amesema wanatarajia
mafunzo hayo yatawapa watafiti hao mbinu bora katika masuala ya kitafiti.
Mratibu wa Teknolojia na Ushauri wa Kitaalam SUA Dkt. Doreen Ndosi akitoa shukrani kwa mgeni rasmi
Amesema kupitia Program ya kuwasaidia watafiti
wachanga ya SUARIS wana imani kubwa kuwa mafunzo hayo yatawapa mbinu bora zaidi
za kufanya tafiti, kuandika miradi ya kitafiti, kutafuta wafadhili wa
miradi na namna bora ya kusimamia miradi
hiyo ili ilete tija.
Picha chini ni watafiti mbalimbali wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi (hayupo pichani)
0 Comments