Na: Calvin Gwabara – Katavi.
Wanataaluma na Wanafunzi katika
Kampasi ya SUA Mizengo Pinda Mkoani Katavi wameupongeza Mradi wa Elimu ya juu
kwa mageuzi ya kiuchumi (HEET) kwa kuwezesha na kuhimiza elimu ya masuala ya
Jinsia katika Taasisi za Elimu Chuoni
kwakuwa inasaidia kufanya mazingira ya Chuo kuwa salama kwa wote.
Bi. Dorothea Clemence Kipangula Mkufunzi Msaidizi katika Kampasi ya SUA Mizengo Pinda akizungumza na SUAMEDIA faida za mafunzo hayo mara baada ya kuhitimishwa Chuoni hapo.
Akionge mara baada ya mafunzo
hayo Mkufunzi Msaidizi katika Kampasi hiyo Bi. Dorothea Clemence Kipangula amesema
mara nyingi watu wamekuwa wakidhani Jinsia ni mambo yanayohusu Mwanaume na
Mwanamke pekee lakini baada ya mafunzo hayo amemejifunza kuwa Jinsia inakwenda mbali na kuwajumuisha watu wenye
ulemavu na mahitaji maalumu.
“Kwahiyo mimi kama Mwalimu
nimejifunza kuwa hata ninapokuwa nafundisha hasa linapokuja kundi jipya la Wanafunzi
mimi kama mwalimu natakiwa kuchukua muda kuwatambua vizuri na kujua ni Mwanafunzi
gani anauhitaji maalumu na nitamfundisha vipi ili aweze kupata kile
anachokitarajia sawasawa na wengine na kutimiza ndoto na malengo yake Chuoni”
Alifafanua Bi. Dorothea.
Aidha amesema kwa mafunzo hayo
yamewafungua macho kama Walimu namna ya kuteleza majukumu yao lakini pia katika
maisha yao ya kawaida na kusaidia kujenga Chuo na Wahitimu wanaotoka katika
Kampasi ya Mizengo Pinda na SUA kwa ujumla wake.
Nae kwa upande wake Mwalimu Neema
Mwawadu amesema amefurahishwa na mpango wa Wizara na Chuo kuanzisha Dawati la
Jinsia ambalo litakuwa linashughulikia maswala yote ya Unyanyasaji na Ukatili
wa kijinsia pamoja na kutoa Elimu sahihi ya masuala hayo ambayo yasipodhibitiwa
yanaweza kuathiri utekelezaji wa majukumu kwa Walimu, Wanafunzi, Wafanyakazi
wengine pamoja na watoa huduma Chuoni hapo.
“Mafunzo haya yatanisaidia sana maana kwanza nafundisha wanafunzi wa Kike na Kiume hivyo wakati nikiwa darasani nitahakikisha hata kwenye kutoa mifano sitoi ambayo inaweza kuathiri kundi lolote ili kila mmoja ajifunze kwa amani na kuona anathaminiwa” alisisitiza Bi. Neema.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti
wa Serikali ya Wanafunzi SUASO Kampasi ya Mizengo Pinda bwana Abihudi Fadhili amesema
wamefurahi sana kupata mafunzo hayo ambayo yameelezea Jinsia kwa mapana yake na
hivyo kuwezesha kujua makossa ambayo wamekuwa wakiyafanya kutokana na matendo
yao ambayo wanayafanya kwa kufahamu au kutokufahamu kuwa ni makossa na kuathiri
maisha ya watu wengine.
“Tumeona ni muhimu kujifunza masuala haya maana itatusaidia kuondoa migogoro mbalimbali kati ya Walimu wetu na Wanafunzi na Wanafunzi, Wanafunzi na Wafanyakazi Lakini pia Wanafunzi na Watoa huduma Chuoni na nitahakikisha nakuwa mstari wa mbele katika kutoa elimu kwa wenzangu wote kwenye Kampasi yetu ya Mizengo Pinda” alieleza bwana Abihudi.
Mradi wa Elimu ya Juu kwa mageuzi
ya kiuchumi (HEET) umewezesha wataalamu na wabobevu wa Masuala ya Jinsia
kufanya mafunzo ya kujenga uwezo kwa Wanataaluma na Wanafunzi kwenye kampasi ya
Mizengo Pinda Mkoani Katavi ili kuwaandaa utekelezaji wa Sera na Miongozo
mbalimbali ya Chuo, Wizara na Kikanda katika kushughulikia masuala yote ya
Jinsia na hivyo kufanya taasisi za Elimu kuwa salama kwa wote.
Kiongozi
wa Masuala ya Jinsia kwenye mradi wa wa Elimu ya juu kwa mageuzi ya kiuchumi
(HEET) Prof. John Jeckoniah akionesha ka mifano baadhi ya picha kwenye Projector zinazoonesha unyanyasaji wa Kijinsia ofisini.
Mtaalamu wa Jinsia na Maendeleo SUA Dkt. Angela Jesse akiwasilisha mada yake kuhusu Miongozo na sheria za SUA,Kitaifa na kimataifa zinazohimiza masuala ya uzingatiaji wa Jinsia . |
Washiriki wa mafunzo hayo ya siku moja yaliyohusisha Walimu, Wanafunzi, Wafanyakazi waendeshaji wakifuatilia mada mbalimbali za masuala ya Jinsia zilizokuwa zikiwasilishwa. |
Washiriki wa mafunzo hayo ya siku moja yaliyohusisha Walimu, Wanafunzi, Wafanyakazi waendeshaji wakifuatilia mada mbalimbali za masuala ya Jinsia zilizokuwa zikiwasilishwa. |
Washiriki wa mafunzo hayo ya siku moja
yaliyohusisha Walimu, Wanafunzi, Wafanyakazi waendeshaji wakifuatilia mada
mbalimbali za masuala ya Jinsia zilizokuwa zikiwasilishwa.
Muonekano wa Mbele geti la kuinia jingo la Utawala la Kampasi hiyo ya SUA ya Mizengo Pinda Mkoani Katavi.
Picha ya Pamoja ya Washiriki wa mafunzo hayo ya jinsia kwenye kampasi ya Mizengo Pinda mkoani Katavi. |
0 Comments