Na: Adam Maruma.
Chama cha Madaktari wa Mifugo Tanzania
(TVA) kimepanga kufanya shughuli mbalimbali za kijamii mkoani Dodoma, ikiwa ni
kuelekea katika Kongamano la Chama hicho litakalofanyika katika ukumbi wa
Hazina mkoani humo kuanzia 5 Desemba, 2022.
Mwenyekiti wa TVA Prof. Esron Daniel Karimuribo akizungumza na SUAMEDIA ofisini. |
Prof. Karimuribo amezitaja chanjo
nyingine zitakazotolewa katika wiki hiyo muhimu kwa Madaktari wa Mifugo kuwa ni chanjo kwa ajili ya kuwakinga Mbuzi na
Kondoo na ugonjwa wa Sotoka unaoshambulia wanyama hao pamoja na chanjo ya Mbwa,
Paka na Punda kwa ajili ya Kuzuia ugonjwa wa Kichaa cha Mbwa kwa wanyama hao.
Kwa upande wa Visumbufu vinavyosababisha
magonjwa kwa mifugo kama kupe na mbun’go Chama hicho cha Madaktari wa Mifugo
Tanzania, kimepanga kutoa elimu kwa wafugaji itakayowawezesha kupambana na
visumbufu hivyo lakini pia kutakua na huduma ya kuogesha mifugo kwa kutumia
josho linalotembea (mobile dip) ili kuweza kuwafikia wafugaji katika maeneo
mbalimbali ya Tarafa ya Mbalawala mkoani humo.
Mwenyekiti huyo ameongeza kuwa
suala la Elimu ya ufugaji bora na wenye tija kwa wafugaji na nchini kwa ujumla litafikiwa endapo elimu ya ufugaji itaanza kutolewa kwa watoto hasa kwenye Taasisi kama Shule za
Msingi na Sekondari na hivyo chama kimejipanga kutoa elimu hiyo kwenye maeneo mbalimbali ya Jiji hilo.
Prof. Karimuribo ameongeza kuwa
suala la matumizi sahihi ya Dawa pia halijaachwa nyuma katika kushajihisha wiki
hiyo na amesema tatizo la matumizi
holela ya dawa za kutibu mifugo inasababisha usugu wa vimelea vya magonjwa
ambayo ni tatizo kubwa kwa wafugaji hivyo pia linapewa nafasi kubwa ya elimu
kwa wafugaji hao.
Huduma nyingine ambayo Mwenyekiti
huyo ameitaja ni huduma ya upasuaji kwa mifugo ili kuzuia idadi ya mifugo kuzaliana kwa kasi na kuongeza kuwa zoezi la hilo la upasuaji
hufanyika ili kuondoa kizazi kwa mifugo jike
au kuhasi kwa mifugo dume na pia
upasuaji hufanyika kwa mifugo kama ng’ombe wanapokua wamekula mifuko ya plastiki
ambayo haisagiki tumboni na hivyo kudhoofisha afya ya ngombe huyo, hivyo
hupasuliwa na kutoa mfuko huo na afya ya mnyama huyo huimarika tena.
Aidha Prof. Karimuribo amesema Kongamano
rasmi la Kisayansi litakua siku ya pili yaani tarehe 6 Desemba, 2022 ambalo
linatarajiwa kufunguliwa rasmi na Waziri wa TAMISEMI Mh. Angela Kairuki na kutakua
na mawasilisho ya Tafiti mbalimbali za Kisayansi
kwa mwaka Mzima kwa siku tatu mfululizo na litakamilishwa na Mkutano Mkuu wa
Chama cha Madaktari wa Mifugo Tanzania TVA.
Mwenyekiti huyo pia amewashukuru
wadau mbalimbali watakaoshiriki kwenye maonesho ya vifaa tiba kwa mifugo, namna
ya kutengeneza vyakula vya mifugo nje ya ukumbi wa kongamano hilo, pia amewashukuru
wale waliowashika mikono kwenye shughuli hiyo kama vile Wizara ya Mifugo na Uvuvi,SUA,TAWIRI,
na kampuni nyingine nyingi.
0 Comments