SUAMEDIA

Wafanyakazi wa Kampasi ya Mizengo Pinda Katavi wakishiriki kutoa maoni kuhusu utekelezaji wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mabadiliko ya Kiuchumi (HEET)

 Na: Tatyana Celestine

Wafanyakazi wa Kampasi ya Mizengo Pinda (SUA) Katavi wameshukuru utaratibu unaofanywa na Mradi wa HEET kwa kuendelea kuwashirikisha wadau wake katika kutoa maoni yao ikiwa ni hatua za awali kabla ya  utekelezaji wa Mradi huo.
Mtaalam wa Mazingira Dr. Amina Hamad (katikati) Mtaalam wa masuala ya Kijamii Prof. David Mhando (kulia) pamoja na Afisa Mipango Bw. Rasauli Karokola (kushoto) wakikusanya mawazo ya Wafanyakazi wa Kampasi ya Mizengo Pinda, Katavi kabla ya kutekeleza Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mabadiliko ya Kiuchumi (HEET).


Wakizungumza katika kikao cha kufanya tathminini kwa Wafanyakazi hao ili kuona wana mawazo gani kabla ya kuanza kwa Mradi ambayo yatakuwa chachu katika kuboresha, kuweka usawa na kuongeza ufanisi katika malengo yanayotarajiwa na Benki ya Dunia.

Afisa Mipango wa Kampasi ya Mizengo Pinda Bw. Rasuli Idrissa Karokola ametoa ufafanuzi  zaidi kuhusiana na Mradi huo ili kuongeza uelewa kwa wafanyakazi na kuona ni jinsi gani ya kuongeza njia ya mawasiliano baina yao ili kupeana taarifa kwa wakati pindi Mradi huo ukiendelea ambao kwasasa wameshaanza kunufaika na  kwa kwenda kusoma.

Akizungumza wakati wa kukusanya maoni kwa Wafanyakazi hao kabla ya mradi huo kuanza Bw. Gabriel Mruma ambaye ni Mfanyakazi kutoka Kampasi hiyo ameeleza kuwa angependa kusikia taarifa zaidi za Mradi huo ili kuweza kutambua nafasi yake ifikapo  awamu ya pili mara baada ya awamu ya wanufaika wa kwanza kukamilika.

Aidha wafanyakazi hao wameorodhesha njia mbalimbali ambazo ni chanya kwao kuweza kupata taarifa halisi iwe moja kwa moja au kutumia njia nyingine kama email, simu, whats app, link katika tovuti ambazo zitaweza kuwafikia watu wa aina zote hata yule ambaye sio Mwanataaluma kutokana na kuwa watendaji mara nyingi hawana utaratibu wa kuingia kwenye mitandao mara kwa mara.

Bw. Karokola amewaasa Wafanyakazi wa Kampasi hiyo kujenga mazoea ya kuingia katika mitandao ili kupata taarifa za chuo zinzowekwa kwani taarifa zote muhimu zinazomuhusu mfanyakazi zinapatikana huko kwa haraka na hata hizo za mradi ziliwekwa huko lakini pia wafanyakazi wote bila kujali ni mtendaji wala mwanataaluma wajenge tabia ya kutaka kujua kitu ambacho kinaweza kuwa na manufaa katika maisha yao wawapo kazini.

Nae Mtaalam wa Mazingira Dr. Amina Hamad amesema kuwa kama Benk ya Dunia inavyotaka mradi huo ufanyike lazima ushirikishwaji uwe wa hali ya juu na kwa hatua kulingana na makundi maalumu yaliyopangwa kwa maana ya kuona kila upande unatoa maoni yake kuhusiana na mradi huo ambapo wadau wakuu ni pamoja na wafanyakazi, wanafunzi, wakazi wazungukao eneo la mradi na wengineo.

Aidha wafanyakazi hao wameshukuru kufika wa mradi huo katika Kampasi ya Mizengo Pinda na kusema kuwa utawasaidia wote kwa ujumla kutokana na kuongezeka kwa Miundombinu kwamba Chuo kitakuwa na miundombinu rafiki hivyo wanafunzi watavutiwa kuja kusoma, kuongezeka kwa huduma za kujamii kwa maanda ya kuwa na fursa za biashara na uwekezaji ndani nan je ya chuo lakini pia kutaongeza uwezo na ufanisi mara baada ya kunufaika kielimu kupitia Mradi.

Katika picha Wafanyakazi wa Kampasi ya Mizengo Pinda Katavi wakishiriki kikao cha  Tathminini katika utekelezaji wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mabadiliko ya Kiuchumi.










Post a Comment

0 Comments