Na: Calvin Gwabara - Mvomero.
Kufuatia
mafanikio makubwa yalioonekana kwenye vijiji vitano vya Halmashauri ya Wilaya
ya Mvomero Mkoani Morogoro vinavyotekeeleza Mradi wa Usimamizi shirikishi wa misitu
na Mkaa endelevu Halmashauri hiyo imetenga kiasi cha shilingi milioni 15
kwaajili ya kuanzisha mfumo huo kwenye vijiji vingine vipya viwili baada ya
mradi kuondoka.
Mkuu wa Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira wa Wilaya hiyo Bi.Merry Massey wakati akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake . |
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira wa Wilaya hiyo Bi.Merry Massey wakati akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake juu ya mafanikio yaliyojitokeza katika kipindi cha miaka yote ya utekelezaji wa Mradi huo kuhifadhi misitu kwa kuwezesha biashara endelevu ya mazao ya misitu Tanzania (CoForEST) kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo na ushirikiano la Uswisi (SDC) Wilayani humo.
Amesema kumekuwa
na mafanikio makubwa kwenye vijiji vinavyotekeleza mradi huo hasa Elimu ya
Uhifadhi kwa jamii na Mapato yatokanayo
na rasilimali za misitu ikilinganishwa
na maeneo mengine ambayo hayapo kwenye mradi huo na wameliona hilo hasa pale
inapotokea jambo lolote la uharibifu wamekuwa wa kwanza kutoa taarifa na
kushughulikia lakini pia utekelezaji wa miradhi ya maendeleo.
“Kwa kuliona
hilo tayari tumeandaa mkakati maalumu na mfuko ambao utatunishwa kupitia fedha
za halmashauri, mapato ya vijiji pamoja na wadau wengine hasa wawekezaji wetu
kupata fedha zaidi za kutelekeza mpango huo wa usimamizi shirikishi na uvunaji
endelevu wa mazao ya misitu na kwa sasa Halmashauri imetenga kiasi cha shilingi
milioni 15 kuanzisha mpango huo kwenye vijiji vipya viwili” alieleza
Amevitaja
vijiji hivyo ambavyo vitaanzishwa na Halmashauri kuwa Kijiji cha Njeula na Matale
na ile asilimia kumi ya mapato inayotoka kwenye vijiji 10 ambayo vinaendesha
mradi huo nayo pamoja na kufanya shughuli za elimu na ufuatiliaji lakini pia
itasaidia kutunisha mfumo huo.
Kwa upane
wake Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya hiyo Dkt. Philipina Philipo amesema Halmashauri
inatambua umuhimu wa mazingira na utunzaji wa misitu maana kupitia misitu na
mazingira mazuri ndipo inapatikana Mvua, Hewa safi na mambo mengine mengi akitolea
mfano kuwa mabadiliko ya tabia nchi kwa sasa yamesababisha viumbe vyote
binadamu na Wanyama kupata tabu nah ii kufika hadi kwenye ekta za uzalishaji
kama vile viwanda kukosa malighafi na umeme kwakuwa maji kwenye mabwawa ya
kuzalisha umeme maji yamepungua.
Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya hiyo Dkt. Philipina Philipo akiongea na Waandishi wa ofisini kwake (Hawapo pichani) |
Dkt.
Philipina ameshukuru jitihada kubwa zilizofanywa na mradi katika kutoa elimu
kwa jamii kuhusu utunzaji wa mazingira na uhifadhi wa misitu na kuboresha
huduma za jamii kwenye vijiji kupitia uvunaji endelevu wa mkaa na mbao kwa
kujenga Madarasa, Zahanati na ofisi za vijiji na hivyo kuifanya jamii kuona
thamani ya misitu yao ya vijiji.
Mradi wa CoForEST
unatekelezwa na Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG) kwa
kushirikiana na Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (MJUMITA) katika
vijiji 35 vilivyopo kwenye wilaya za Morogoro, Kilosa na Mvomero mkoani
Morogoro, Liwale, Ruangwa na Nachingwea mkoani Lindi na Kilolo mkoani Iringa.
Waandishi wa habari kutoka vyombo vya habari mbalimbali nchini wakifuatilia mkutano huo namaelezo kutoka kwa viongozi wa Wilaya hiyo. |
Waandishi wa habari kutoka vyombo vya habari mbalimbali nchini wakifuatilia mkutano huo namaelezo kutoka kwa viongozi wa Wilaya hiyo. |
0 Comments