Winfrida Nicolaus
Kupitia Maonesho ya 29 ya Wakulima, Wafugaji na
Wavuvi Kanda ya Mashariki, Shule Kuu ya Uhandisi na Teknolojia SUA imeandaa na
kuonesha Teknolojia ya kisasa ya Umwagiliaji kwa njia ya simu pamoja na Ndege bila
rubani shambani.
Amesema Teknolojia ya Simu inamuwezesha Mkulima
ambaye ameshindwa kufika shambani kutokana na shughuli nyingi za hapa na pale
kumwagilia bila yeye kuwepo shambani kwa kutuma meseji ya neno mwagilia na
mfumo unajifungua na kuanza kumwagilia na akihitaji kuufunga anatuma neno funga
au zima na unajifunga wenyewe moja kwa moja.
Bw. Reuben amesema Teknolojia hiyo ya
Umwagiliaji kwa njia ya simu itamjulisha mkulima pia endapo maji ya kumwagilia
yameisha ambapo utamsaidia kuweza kutafuta namna ya kuweka maji na shughuli ya
umwagiliaji kuendelea katika shamba lake.
Amesema Teknolojia nyingine ni matumzi ya Ndege
bila Rubani Shambani ambayo inauwezo wa kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa ambapo
inaweza kumtaarifu Mkulima kama mbolea imepungua kwenye zao lake na kumfanya
ajue kiasi gani cha mbolea kinahitajika kulingana na upungufu na kuweza kuweka
mbolea mahali sahihi.
“Mkulima anacho kifanya akiwa eneo lolote hata
nje ya nchi anaweza akaamuru mfumo ufanye anachokihitaji kifanyike shambani na
kitafanyika iwe kumwagilia au kumjulisha changamoto zilizopo shambani mfano
maji yameisha”, amesema Bw. Reuben
Aidha amesema hapo baadaye wataanza kutumia
Sensa ambazo zitawekwa shambani na zinauwezo wa kusema kiasi cha unyevunyevu
ulioko kwenye shamba ambapo mfumo una uwezo wa kujiseti wenyewe na kutoa
taarifa.
Naye Fundi Sanifu wa Zana za Kilimo katika Shule
Kuu ya Uhandisi na Teknolojia SUA Bakari Mohamed amesema katika Maonesho hayo wanatambulisha
pia Shule ya Udereva wa Magari, Pikipiki pamoja na Uendeshaji wa Mitambo ya
Kilimo kama vile Matrekta, Makatapila, Mitambo ya kuvunia mahindi na mengineyo.
Amesema kuna faida kubwa endapo mtu atajifunza
Udereva kutoka SUA kwasababu wanatoa elimu kwa Vitendo kutokana na kuwa na
vifaa vyote ikiwemo mitambo yenyewe na elimu inatolewa kwa bei nafuu na
mwanafunzi atajifunza kwa muda mfupi pia mwanafunzi hawezi kumaliza mafunzo
bila kufanyiwa majaribio na Askari wa Usalama barabarani ambapo itampelekea
leseni yake kuwa bora zaidi.





0 Comments