SUAMEDIA

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatma Mwasa amekiomba SUA kuanza kubadili mtazamo kuhusu Kilimo ili elimu wanayoitoa ianzie kwa jamii ya Morogoro


Na: Tatyana Celestine                     

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatma Mwasa amekiomba Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kuanza kubadili mtazamo kuhusu kilimo ili elimu wanayoitoa ianzie kwa jamii ya Morogoro moja kwa moja na kuwafikia wananchi kikamilifu.




Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Bi Fatma Mwasa akiangalia bidhaa mbalimbali katika Banda la SUA katika Maonesho ya 29 ya Nanenane mkoani Morogoro.


Mkuu wa Mkoa huyo amesema hayo mara baada ya kutembelea Banda la SUA Agost 3, 2022 na kujionea Teknolojia na Tafiti mbalimbali za Kilimo katika banda hilo ikiwa ni siku moja kabla ya Mgeni rasmi kufungua Maonesho hayo.

Mhe. Fatma amesema Serikali itaandaa kikao kitakacho jumuisha Wadau wa Kilimo, Watafiti na Viongozi wa Mkoa kwa pamoja na Wagani wa Wilaya zote za mkoa wa Morogoro ili kujadili namna nzuri ya kuifikisha elimu hiyo inayotolewa na SUA kwa jamii.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa amesema lengo la kuitisha kikao hicho litakuwa ni kujadiliana na kupeana maarifa zaidi yatakayowezesha kutambua na kujipanga vizuri katika Sekta ya Kilimo ili sekta hiyo iweze kuwa na tija.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa amekipongeza Chuo cha SUA kwa kuwezesha watu kujifunza kutokana na Tafiti na Teknolojia mbalimbali za kilimo katika Maonesho ya 29 ya Nanenane Kanda ya Mashariki yanayofanyika mkoani Morogoro.


Hii ni mara ya kwanza kwa Mkuu wa mkoa huyo kutembelea Banda la SUA katika Maonesho ya Nanenane tangu kuteuliwa kwake kutumikia nyadhifa hiyo.











KATIKA VIEDEO MKUU WA WILAYA AKIJIBU SWALI MARA BAADA YA KUULIZWA NA SUAMEDIA KATIKA VIWANJA VYA NANENANE MKOANI MOROGORO

Post a Comment

0 Comments