Na Amina Hezron, Morogoro
Katika kuhakikisha Wakulima
wanakabiliana na mabadiliko ya tabianchi katika kilimo nchini Chuo Kikuu cha
Sokoine cha Kilimo SUA kimetoa mafunzo ya matumizi ya Matandazo katika kilimo
kwa Wakulima wa zao la Maharage kutoka Kijiji cha Ndole Wilaya ya Mvomero
mkoani Morogoro.
“Moja kati ya tandazo ambalo
tumelionesha ni tandazo la aina kama ya plastiki kutoka kiwandani ambalo
likikaa mwaka mmoja shambani linaoza, tumetumia tandazo hili ili tuweze kuona
ubora wake na ubora wa yale matandazo ya asili, hivyo tumewaleta wakulima ili
wao wenyewe waweze kuangalia na kutoa maamuzi ya aina gani ya matandazo
wanaweza wakayatumia na hii ni baada ya wao kufanya tathimini kuona namna
wanaweza kuyapata”, alisema Prof.
Msolla.
Akielezea uzoefu wake katika
kilimo mmoja ya Wakulima Daudi Tesha amesema kuwa pamoja na kugundua kuwa
matandazo yanaongeza mavuno wakati mwingine imewalazimu kulima Maharage pasipo
kutumia matandazo na hiyo ni kutokana na changamoto ya upatikanaji wa matandazo
hayo.
“Kule kijijini sehemu ambayo tunalima kwa
matandazo majani yanakuwa si mengi kama kule ambako tunalima bila matandazo
nimefurahi leo nimepata mbinu mpya ya kukabiliana na uhaba wa matandazo kwamba
naweza kutumia matandazo ya kiwandani na yakanisaidia katika kilimo hivyo
niombe tu elimu hii iweze kuwafikia na Wakulima wengine wa vijijini ambao
hawakupata fursa ya kuwa hapa leo ili na wao wakanufaike”, alisema Tesha.
Naye Mkulima mwingine Estelia
Venas amesema kuwa katika mafunzo hayo amejifunza njia mpya kabisa ambazo
alikuwa hazifahamu hivyo matarajio yake mara baada ya kutumia njia hiyo
mpya ya matandazo ya kiwandani
anategemea kupata mavuno zaidi yatayokwenda kumkomboa kiuchumi.
Kwa upande wake Mkulima Kimweli Julius ambaye ni mara ya pili
kupata mafunzo kutoka SUA ameeleza kuwa awali walikuwa wakilima na kupanda
mazao pasipokuzingazia umbali wa shimo kwa shimo akapata elimu ya namna sahihi
ya upandaji na ameona matunda mazuri ya kufuata njia hiyo.
“Lakini kwa sasa changamoto
iliyopo ni majani ambayo yanakuwa mengi sana shambani na suluhisho ndio hilo
nimefundishwa leo hivyo nakwenda kulifanyia kazi ili nami niweze kupata manufaa
yale niliyoyaona katika shamba darasa”, alisema Julius.
.jpg)
.jpg)
0 Comments