Na,Winfrida Nicolaus
Wanafunzi wa Shahada ya Uzamili
pamoja na wanafunzi wa Shahada ya Uzamivu kutoka kitengo cha Sayansi ya Mimea Ndani
ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) wameendelea kufanya tafiti kwenye mradi
unaolenga kuzalisha Mbegu Vumilivu ya
Mpunga kwa Mabadiliko ya Tabia Nchi (CLIMATE-SMART AFRICAN RICE) huku lengo likiwa
ni kuwajengea uwezo na kuleta majibu ya tafiti zenye tija kwa maendeleo ya nchi
Hayo yamesemwa na
Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania TARI Dkt. Atugonza Bilaro wakati wa mkutano wa siku tatu uliofanyika
SUA naa kuendeshwa na washiriki toka Chuo Kikuu cha Copenhagen kilichopo nchini
Denmark, Taasisi ya Utafiti wa Mpunga IRRI, Taasisi ya Utafiti wa Kilimo
Tanzania TARI pamoja na SUA ambao ndio wasimamizi wakuu wa mradi huo.
Dkt. Bilaro amesema kuwa ili
kufikia uzalishaji wa mpunga wenye tija ni mchakato na wao kama wataalam
wameona ni bora zaidi kuwatumia wanafunzi kwa kuwa watafanya kwa vitendo hatua
kwa hatua hadi kufikia lengo la mradi huo la kuzalisha mbegu ya mpunga yenye
tija na stahimilivu kwa mabadiliko ya tabia nchi
Amesema kupata watafiti
wazuri kunahitaji jitihada za kutosha na jitihada hizo zipo katika kuwaandaa
wanafunzi hao mapema kwa kuwashirikisha katika miradi mbalimbali katika kile
wanachosomea ili waweze kuwa bora na hata kuaminiwa kutokana na uzoefu
walionao.
‘‘Kwa
hiyo nataka tu kusema wanafunzi hawa tunaowatumia katika mradi huu ndio hao
watakuja hata katika mashirika yetu kwaajili ya kufanya kazi ingawa wengine ni
wafanya kazi tayari hivyo basi watatusaidia kufanya kazi zenya tija na kuleta
maendeleo kwa taifa kwasababu kwanza kabisa tunataka kufanya zao la mpunga kuwa
la kibiashara hivyo bas mpaka kukamilika kwa mradi huu ambao utaendeshwa kwa muda
wa miaka mitano ambao utawafanya kuwa bora zaidi’’. Amesema Dkt.
Bilaro
Kwa upande wake Afisa Kiungo kati ya Serikali ya Tanzania na Shirika la
Kimataifa la Utafiti wa Mpunga IRRI Bwana George Iranga amesema ushirikiano wa
shirika la kitaifa la Utafiti wa Mpunga IRRI pamoja na SUA umeleta mafanikio
mazuri sana katika sekta ya kilimo hivyo hatua iyo ya kushirikisha wanafunzi
toka chuoni hapo katika mradi kutaleta ongezeko la watafiti wazuri na wenye
uzoefu katika kutatua changamoto za wakulima nchini.
‘‘tupo hapa kama
washirika ambao tumeshirikiana na Chuo Cha Sokoine Cha Kilimo SUA katika mradi
huu ambao mpaka sasa una miaka miwili na unasehemu ya kuwafundisha wanafunzi
katika levo ya uzamili, uzamivu Pamoja na kutoa kozi fupi katika kuwajengea
uwezo ili waweze kutatua changamoto za wakulima hasa katika changamoto hii ya
mabadiliko ya hali ya hewa kwa kuleta mbegu stahimilivu kwa kila mabadiliko ya
tabia nchi na zenye tija’’.
Amesema Bwana George Iranga
0 Comments