SUAMEDIA

Rais Samia ashiriki kumbukumbu Kifo cha Karume

 RAIS Samia Suluhu Hassan, ameshiriki katika dua maalum ya kumbukumbu ya kifo cha Rais wa Kwanza wa Zanzibar, hayati Abeid Amani Karume.


Baadhi ya viongozi wengine waliohudhuria kumbukumbu hiyo ni Makamu wa Rais, Dk. Philip Mpango, Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi, Mkuu wa Majeshi, Jenerali Venance Mabeyo, Rais mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume na mjane wa hayati Karume, Fatma Karume.

 Viongozi hao pamoja na wananchi wengine walishiriki katika dua ya pamoja Ofisi Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Kisiwandui, Zanzibar eneo lilipo  kaburi la hayati Karume. Mzee Karume aliuawa kwa kupigwa risasi Aprili 07, 1972, ambapo leo imetimia miaka 50 tangu tukio hilo litokee.


Post a Comment

0 Comments