Gerald
Lwomile
Dodoma
Chuo Kikuu cha Sokoine
cha Kilimo (SUA), Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Shirika la ‘International Centre
for Antimicrobial Resistance Solutions’ (ICARS) la Denmark wameingia
makubaliano ya kufanya utafiti wa kutumia chanjo na usafi katika kuthibiti
magonjwa ya kuku nchini ili kupunguza matumizi ya dawa hususani dawa za antibiotiki
ili kulinda afya za walaji.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulege kushoto akimakaribisha Prof. Robinson Mdegela ofisini kwake Jiji Dodoma
Akizungumza mara baada ya kupokea taarifa ya namna miradi miwili ya utafiti utakavyofanyika hapa nchini, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulege amesema kama utafiti huo utafanyika vizuri utaleta matokeo chanya kwa wafugaji ambao watatumia usafi na chanjo na kupunguza matumizi ya dawa kwenye kuku.
Awali akizungumza
wakati akitoa taarifa ya miradi hiyo Mtafiti Kiongozi na Mhadhiri Mwandamizi
kutoka SUA Prof. Robinson Mdegela amesema SUA na Wizara Mifugo na Uvuvi
wameandika miradi miwili ya utafiti ambayo ni uwezekano wa kutumia njia za usafi
kwenye mabanda ya kuku na kuchanja kuku
ili kudhibiti magonjwa ya kuku hivyo kupunguza matumizi ya madawa yasiyo ya
lazima.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa ICARS Bibi. Helle Engslund Krarup kushoto akisaini makubalino ya kuanza kwa miradi hiyo, kulia ni Prof. Mdegela kutoa SUA
Prof. Mdegela amesema matumizi
hayo yamesababisha vifo vingi duniani kote na inakadiriwa hadi kufikia mwaka 2050
zaidi ya watu milioni kumi wako hatarini kufa kutokana na matumizi ya mazao ya
kuku kwa kula mabaki ya dawa ambayo madhara yake ni pamoja na usugu wa vimelea
kwenye dawa.
“……, tunayo furaha kuwa
shirika hili la ICARS la Denmark limekubali kufadhili miradi hii miwili kwani ukweli
ni kuwa upo ushahidi matumizi ya mabaki ya dawa yanaleta madhara pamoja na
usugu wa vimelea jambo linalohatarisha Maisha ya walaji” Amesema Prof. Mdegela
Naye Mkurugenzi wa Uendeshaji
wa ICARS Bibi. Helle Engslund Krarup amesema na
ukweli usio na shaka kuwa matumizi ya antibiotiki zitokanaza na mabaki ya dawa kwenye mazao ya kuku ni
tatizo kubwa duniani kote ambapo hadi kufikia mwaka 2019 zaidi ya watu milioni
5 walikufa huku nchi zilizoko Kusini mwa Afika zikipoteza zaidi ya watu laki
mbili na elfu hamsini
“Serikali ya Denmark
ikaona ni vyema Shirika hili la ICARS lifanye kazi na washirika wake ili kupata
suluhisho la namna gani hali hii inaweza kudhibitiwa na kuwa tunayofuraha kufanya
kazi na Wizara ya Mifugo na Uvuvi na SUA” amesema Bibi. Krarup
0 Comments