Idara mpya ya Uhandisi Ujenzi na Rasilimali za Maji ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA imepokea vifaa vipya vyenye thamani ya zaidi ya Euro elfu 83 ambazo ni sawa na zaidi ya sh. Million 224.4 kutoka serikalini kupitia Wizara ya Elimu ambavyo vitasaidia kuongeza ufanisi.
Mteknolojia Mwandamizi kutoka Idara hiyo Dkt. Paul Reuben amesema ujio wa vifaa hivyo utaongeza ufanisi wa utendaji kazi katika ufundishaji, utafiti,usimamizi wa miradi ya maendeleo kwa sekta za serikali na mashirika binafsi pamoja na ushauri wa kitaalamu.
‘’Tunaishukuru sana Serikali inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa
kutoa kipaumbele kwenye mafunzo kwa vitendo, hii itafanya wahitimu wawe na
ujuzi na maarifa hivyo kuweza kujiajiri wenyewe wanapokuwa wamemaliza
masomo yao”,alisema Dkt Reuben.
Dkt. Reuben amesema upatikanaji wa vifaa hivyo ni mwanzo wa kuimarisha Idara ambayo itatakiwa kuwa na maabara nyingine ili kuwezesha kufanyika kazi zote za vipimo vya vifaa vya ujenzi ndani ya maabara na sehemu mbalimbali ambako ujenzi unafanyika.
‘’Awali wanafunzi iliwalazimu kusafiri kwenda Vyuo vingine kama vile Chuo Kikuu
cha Dar es salaam (UDSM) kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo huku masomo
mengine ikiwalazimu kufanya kwa nadharia zaidi kuliko vitendo”, ameeleza Dr.
Reuben.
Mteknolojia huyo amesema vifaa hivyo pia vitasaidia wahitimu kupata ajira kwa urahisi pindi wanapohitimu masomo yao.
Kifaa kinachotumika kupima tabia ya udongo kutokana na mgandamizo ili kujua uwezo wa udongo kustahimili mzigo juu yake kama majengo nk (Triaxial Machine). |
Kifaa cha kupima ubora wa matofali na zege kwa ajili ya ujenzi (Compression Machine). |
0 Comments