SUAMEDIA

Makombora ya Urusi yapiga Mji wa Pili kwa ukubwa Ukraine

 


Takriban watu 10 wameuawa na wengine 20 kujeruhiwa baada ya shambulio la kombora kupiga kwenye mji wa pili kwa ukubwa Kharkiv mashariki mwa Ukraine.Makumi ya watu  wengine waliokolewa kutoka chini ya vifusi. 

Picha za video zilionesha kombora likipiga jengo la serikali ya mtaa na kulipuka, na kusababisha moto mkubwa. Kharkiv imekuwa imeshambuliwa kwa mabomu kwa siku kadhaa sasa. 

Post a Comment

0 Comments