Shirika la mpango wa chakula Duniani la Umoja wa Mataifa
linasema eneo la sahel barani Afrika linakabiliwa na ukosefu wa usalama wa
chakula ambao haujawahi kushuhudiwa unaosababishwa na kupanda kwa bei, harakati
za kigaidi, mahitaji makubwa ya kikanda na COVID-19. Mwakilishi wa WFP nchini
Birkina Faso anaonya kwamba hali ni mbaya huku mamilioni ya watu watakabiliwa
na njaa katika miezi ijayo.
Katika maeneo makubwa ya Burkina Faso, vikundi vya kigaidi
vyenye uhusiano na Islamic State na al-Qaida hutembea kwa uhuru mashambani,
wakishambulia raia pamoja na vikosi vya usalama.
Mchanganyiko wa vigezo mbali mbali vibaya unasababisha bei ya
chakula kupanda katika eneo lote, kulingana na program ya chakula duniani
(WFP).
Wizi wa mifugo unaofanywa na makundi ya kigaidi, ni sababu
mojawapo, anasema Antoine Renard, mkurugenzi wa WFP nchini Burkina Faso.
“Kuna mahitaji makubwa katika kanda, kwa hivyo hicho ni
kipengele kimoja katika suala la mwelekeo wa soko. La pili, ni migogoro na bila
shaka ina athari namna ya jinsi unavyoweza kuvuna. Una weza vipi kuendelea
kuhakikisha kwamba masoko yako juu na yanaendelea na biashara huko Burkina
Faso. Na mwisho, ni athari za kiuchumi za COVID-19”.
WFP inasema rekodi inaonyesha watu milioni 28 wana ukosefu wa
usalama wa chakula huko Afrika magharibi na kati.
Pia inasema nchini Burkina Faso, Mali na Niger, njaa inaweza
kuongezeka kwa asilimia 50 katika miezi ijayo, kutoka milioni 5.5 hadi zaidi ya
milioni 8.
0 Comments