SUAMEDIA

Dk Mwinyi afanya uteuzi Wizara ya Utalii

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Mwinyi ameteua viongozi mbalimbali katika Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale.


Taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Zanzibar,   Jumanne Desemba 21, 2021 kwa vyombo vya habari na kusainiwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Zena Said imesema Dk Abdalla Mohamed Juma ametuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Utalii.

Maryam Mohammed Hamid Mansab ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Makumbusho na Mambo ya Kale na Hafsa Hassan Mbamba ameteuliwa kuwa Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya utalii.

"Mohamed Mansour Nassor ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Masoko, kamisheni ya Utalii," imesema

Pia taarifa hiyo imemtaja Aviwa Issa Makame kwamba ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara Rasimali watu, Mipango na utawala, kamisheni ya utalii.

CHANZO MPEKUZI

Post a Comment

0 Comments