SUAMEDIA

Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili TAMISEMI, TBC,TIRDO,TASAC, TAEC, NEC & Wizara ya Maliasili na Utalii

 

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Wizara ya Maliasili na Utalii, Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO), Shirika la Wakala wa Meli Tanzania (TASAC), Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) anapenda kuwataarifu waombaji Kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 13 – 18 Novemba, 2021 na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo.

Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-
i. Usaili utafanyika 13 – 18 Novemba, 2021 kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili; muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada;
ii. Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa Barakoa (Mask);
iii. Kila msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;
iv. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga kura, Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Uraia au Hati ya kusafiria;
 

==>>Kutazama Ratiba na Majina ya Walioitwa kwenye Usaili,BOFYA HAPA.

v. Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV, VI, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji;
vi. Wasailiwa watakaowasilisha“Testimonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hatiza matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI;
vii. Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi.

==>>Kutazama Ratiba na Majina ya Walioitwa kwenye Usaili,BOFYA HAPA.

 ==>>Kupata matangazo ya nafasi mbalimbali za Kazi,BOFYA HAPA.

 

Post a Comment

0 Comments