Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI Prof.Riziki Shemdoe ameridhia kufanyika kwa uhamisho wa watumishi 364 wa kubadilisha vituo vya kazi kwenye Mamlaka za Serikaliza Mitaa.
Prof.Shemdoe amesema kuwa Ofisi ya Rais-TAMISEMI itaendelea kufanyia kazi maombi ya uhamisho wa aina hiyo tu kwa sasa wakati tathmini ya mahitaji ya watumishi kwenye Halmashauri zote ikiendelea kufanyika.
Pia amewakumbusha watumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuwa uhamisho katika Halmashauri za Majiji, Manispaa na Miji kwa sasa umesitishwa mpaka hapo itakapotangazwa vinginevyo.
Aidha amewataka watumishi waliopata vibali vya uhamisho kusubiria barua kwenye Halmashauri zao na sio kuja Ofisi ya Rais-TAMISEMI kufuata barua hizo.
0 Comments