Na Gerald Lwomile
Mwanza
Katika kuadhimisha Miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Chuo
Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Mwalimu
Nyerere na Chuo Kikuu cha Mt. Augustine (SAUT) tarehe 01 Desemba, 2021
kinatarajia kufanya Kongamano la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania
Bara katika Chuo Kikuu cha SAUT Jijini Mwanza
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Prof. Raphael Chibunda akimuonyesha teknolojia mbalimbali Dk. Dolphine Kessy Mhadhiri SAUT aliyevaa miwani katikati
Akizungumza leo Novemba 30, 2021 katika mkutano wake
na waandishi wa habari Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Prof.
Raphael Chibunda amesema Kongamano hilo litajadili mada mbalimbali ikiwemo
maendeleo ya kilimo nchini
Prof. Chibunda amesema katika miaka 60 ya Uhuru wakulima
wa Tanzania wamefanya kazi kubwa katika kuhakikisha wanashiriki kikamilifu
katika uzalishaji wa mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi na hivyo kupelekea taifa
kukabiliana na upungufu wa chakula unapojitokeza
Prof. Chibunda katikati waliokaa mbele akizungumza wa waandishi wa habari kulia kwake ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Utafit na Ushauri wa Kitaalamu Prof. Maulid Mwatawala
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo
ameendelea kusema kuwa uzalishaji bora wa nyama unaofanywa na wafugaji nchini
pia umesaidia kuwepo kwa nyama wakati wote
Akizungumzia suala la uvuvi Prof. Chibunda amesema
watafiti nchini wakiwemo wale wa SUA wameendelea kuhakikisha wanakabiliana na
magonjwa ya Samaki lakini pia kuongeza uzalishaji wa Samaki kwa kuzalisha
vifaranga bora na kuinua lishe na pato la mwananchi
Prof. Chibunda amesema katika kuhakikisha kongamano
hilo linajadili kwa undani maendeleo ya kilimo nchini wamechagua kauli mbiu
isemayo “Mchango wa Sekta ya Kilimo Katika Maendeleo ya Tanzania: Mafanikio na
Changamato Baada ya Miaka 60 ya Uhuru”.
Aidha SUA katika kuitikia wito wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeanza maonesho katika Chuo cha SAUT ambapo inaonesha teknolojia na ubunifu mbalimbali unaofanyika SUA.
KATIKA VIDEO
0 Comments