SUAMEDIA

Makamu Mkuu Chuo Kikuu SUA Prof. Raphael Chibunda, azindua chanjo ya COVID 19

 Na Gladness Mphuru

Makamu Mkuu  Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Prof. Raphael Chibunda, amezindua chanjo ya COVID 19 aina ya Janssen dozi mia tano (500) chuoni hapo, ikiwa ni muendelezo na utekelezaji wa kampeni ya Taifa ya chanjo dhidi ya ugonjwa huo.



Prof. Chibunda amefanya uzinduzi huo akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali wa taasisi hiyo, akiwemo Naibu Makamu Mkuu wa Chuo upande wa Taaluma Prof. Maulid Mwatawala, Makamu Mkuu wa Chuo Utawala na Fedha Prof. Amandus Muhairwa na Daktari mkazi wa Hospitali za SUA Dkt. Omary Kasuwi.

Prof. Chibunda amesema kutokana na Jamii inayoizunguka taasisi hiyo, ikiwemo Jumuiya ya Wanafunzi na Wafanyakazi kufikia takribani watu elfu 20, ndio sababu kubwa ambayo imepelekea kufanyika kwa juhudi za kutuma maombi mkoani ili jumuiya hiyo iwe salama.

“Tumefanya juhudi kubwa kwa watu wa mkoani angalau na sisi watuhusishe kama kituo, sababu kubwa ya kupeleka maombi hayo ilikuwa kwanza kuna watu wengi tunaoishi pamoja, na katika Manispaa hii ya Morogoro hakuna taasisi yenye watu wengi kama SUA” amesema Chibunda

Prof. Chibunda amesema jambo jingine lililopelekea kuomba kupata chanjo hiyo ni kuwa pamoja na kutaka kuchanja katika maeneo yaliyopangwa lakini ilionekana watu kutoka SUA katika cha sabasaba walikuwa ni wengi na hiyo ilionyesha jinsi taasisi hiyo ya kisayansi ilivyoamua kupata chanjo hiyo ya UVICO 19.

Naye Makamu Mkuu wa Chuo Utawala na Fedha Prof. Amandus Mwairwa, amewaasa wanajumuiya wa SUA na watanzania kujitokeza na kuacha ubishi juu ya chanjo sanjari na kuepuka upotoshaji wa chanjo hasa kwenye mitandao ya kijamii, bali wasikilize maelekezo yanayotolewa na wataalamu wa Afya.

Awali akizungumza katika zoezi hilo la chanjo Daktari Mkazi wa Hospitali za SUA Dkt. Omary Kasuwi, amesema wimbi la kwanza la virusi vya CORONA vilivyoanza mnamo mwaka 2019 na 2020 ilikuwa kipindi kigumu kwa Hospitali ya SUA, kwani walipokea takribani watu 2000 wenye maambukizi na watu 5 kati yao walifariki.

“Cha msingi tunaweza tukajifunza nini kimetokea duniani na hasa ulaya, vifo vilivyotokea 2019 na 2020 na idadi ya vifo katika kipindi cha mwezi januari kwa mwaka 2021 unaweza kuona kulikuwa na ongezeko kidogo nah ii inaonyesha kirusi hiki cha ‘Delta’ ni hatari sana” amesema Kasuwi

PICHA ZA VIONGOZI MBALIMBALI SUA WAKIPATIWA CHANJO YA UVICO 19.

Post a Comment

0 Comments