Na.Vedasto George/Winfrida Nicholaus.
Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu
cha Sokoine cha Kilimo SUA kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Copenhagen nchini
Denmark kupitia Mradi wa Mabadiliko ya Vijiji kuwa Miji RAT, umebaini kuwa
asilimia 17 zinatupa taka ngumu kwenye maeneo madogo, huku asilimia 70 ya kaya
zinahifadhi taka kwenywe misombo ambayo ni madampo ya nyumbani.
Hayo ya mebainishwa na Dr.
Eveline Lazaro ambaye ni Mtafiti Kiongozi wa Mradi wa Ukuwaji wa Vijiji kuwa
Miji, ambapo amesema kuwa utafiti huo umefanyika kwa kipindi cha miaka kumi kwa
kushirikiana na Chuo Kikuu cha Copenhagen cha nchini Denmark, lengo likiwa ni
kuangalia changamoto na fursa zilizopo katika ukuaji wa Vijiji kuwa Miji.
Kwa upande wake Prof. Ezron
Karimuribo Mkurugenzi wa Uzamili na Utafiti Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo
SUA, amesema miji inayoibukia mingine kiholela inabidi ikue, ili iweze kuwa na
mamlaka kamili ya miji na iwe na utawala pamoja na muongozo mzuri, na ambao
unaendana na matakwa ya nchi.
Naye Dr. Mukuki Hante Mkurugenzi
Uendelezaji Miji na Vijiji kutoka ofisi ya Raisi TAMISEMI, amesema kuwa miji
inayokua iko zaidi 1454 kwa nchi nzima.
Aidha Prof. Fortunata Makene Mkuu
wa Kitengo cha Utafiti Mkakati na Machapisho kutoka taasisi ya Economic and
Social Research Foundation ESF, amesema miji imekuwa ikikua kwa kasi kuliko
serikali ambavyo imejiandaa katika upangaji wa miji.

0 Comments