SUAMEDIA

Tumieni Jeshi la Zimamoto kumaliza majanga ya Moto


Na.Vedasto George/ Nana Ng’hwaya.

Imeelezwa kuwa ujenzi wa majengo yasiyo fuata taratibu na ushauri kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, ni chanzo kikubwa ambacho kinapelekea kuwepo kwa matukio ya moto, ambayo yanatokea na kughalimu maisha ya watu nchini.




Kauli hiyo imetolewa Mei 17, 2021 na Kamishna wa Utawala na Fedha kutoka jeshi la hilo nchini Mbaraka Semwanza, katika ufunguzi wa maadhimisho ya wiki ya zimamoto na uokoaji, ambayo yamefanyika kitaifa Mei 17 mkoani Morogoro, yakiwa na kaulimbiu isemayo “Shule zetu ni chimbuko la maarifa tuzilinde dhidi ya majanga ya moto”

Aidha Semwanza amewataka wananchi kuwa na tabia ya kutoa taarifa sahihi na kwa wakati, juu ya uwepo wa matukio ya moto kabla ya madhara hayajawa makubwa,  ili jeshi la zimamoto na uokoaji liweze kufika kwa wakati nakuweza kutatua changamoto.

Akifungua maadhimisho hayo kaimu Katibu Tawala kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Bw.Herman Tesha, amelitaka jeshi hilo kufanya kazi kwa weledi bila kujali changamoto zilizopo, na kuongeza kuwa serikali itaendelea kutatua changamoto zinazolikabili jeshi hilo, ikiwemo kuwawezesha vifaa ambavyo vitakuwa na uwezo zaidi katika majanga ya moto.







Bw.Herman Tesha amebainisha kuwa, serikali ya mkoa wa Morogoro kwa kushirikiana na Jeshi la Zimamoto, itaendesha zoezi maalumu la ukaguzi wa shule zote za msingi na sekondari, ikiwa ni jitihada zakuchukua taadhari dhidi ya majanga ya moto.

Maadhimisho ya wiki ya zimamoto na uokoaji yamezinduliwa kitaifa Mei 17 mkoani morogoro na yatafikia kilele chake Mei 21, 2021.





Post a Comment

0 Comments