Na Gladness Mafuru
Imeelezwa kuwa mfumo wa Afya
data hivi sasa umeanza kutumiwa na nchi jirani kama Mozambique wakishirikiana
na Wakfu wa Utafiti na Udhibiti wa Magonjwa Ambukizi ya afya moja wa SACIDS
kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA.
![]() |
| Picha kutoka Maktaba |
Hayo yameelezwa na Afisa
Mawasiliano wa SACIDS Yunus Karsan April 28,2021 wakati akizungumza na
SUAMEDIA ofisini kwake.
Karsan amesema hivi sasa tayari timu ya SACIDS kutoka SUA ipo Mozambique kwa ajili ya kutoa mafunzo ya namna ya kutumia mfumo wa Afya Data katika kukusanya taarifa za magonjwa kutoka kwa jamii wanyama na binadamu.
Ameongeza kuwa mfumo huo wa
Afya Data una wigo mpana wa kutumika ulimwenguni kutokana na
kuwa unaweza kubadili lugha kutokana na mahitaji ya eneo husika.
Aidha ametoa wito kwa wanafunzi
wa SUA kwa ngazi za Uzamili na Uzamivu kujitokeza kwenye nafasi za kwenda
kusoma nje ya nchi pamoja na kufanya tafiti katika vyuo washirika kama
vile NSG iliyopo South Afrika, Uingereza na Korea.

0 Comments