Na: Farida Mkongwe
Waziri wa
Viwanda na Biashara Mhe. Geoffrey Mwambe amemuelezea Hayati Dkt. John Pombe Magufuli
kuwa ni Kiongozi aliyekuwa na mtazamo mpana kiuchumi na ndio maana Nchi ya Tanzania iliingia mapema kwenye uchumi wa kati.
Picha na Star and Stripes |
Mhe. Mwambe ameyasema hayo mapema leo asubuhi Machi 25,2021 kupitia Azam TV wakati akizungumza kwenye Viwanja vya Magufuli wilayani Chato kabla ya wananchi hawajaanza kutoa heshima zao za mwisho kwa Hayati Magufuli.
Waziri
Mwambe amesema ana imani kupitia uongozi wa Rais wa sasa Mhe. Samia Suluhu
Hassan na mipango yote ya Serikali kuhusu suala la viwanda itazidi kusonga mbele
kwa kuwa Mama Samia alikuwa akishirikiana kwa karibu na Hayati Magufuli.
Amesema
wananchi hawana sababu ya kuwa na wasiwasi kwa kuwa Rais Samia Suluhu Hassan
ataendelea kuyasimamia, kuyaenzi na kuongoza kama ambavyo alikuwa akifanya
Hayati Dkt. Magufuli.
Kuhusu
suala la kuyaendeleza masoko na wajasiriamali, Mh. Mwambe amesema tayari
ameshatoa maelekezo kwa Taasisi ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzanai
TAN-TRADE kuongeza juhudi za kimkakati kuhakikisha masoko yaliyofunguliwa
yakiwemo ya Afrika Mashariki yanaendelezwa ipasavyo.
-30-
0 Comments