SUAMEDIA

Wafanyakazi na wanafunzi toeni taarifa za ukiukwaji wa uadilifu. Hata hivyo, taarifa hizo zisiwe za majungu - Prof Mahonge

 

Na Gerald Lwomile

Katavi

Wafanyakazi na wanafunzi katika Kampasi zote za Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) wameshauriwa kutokuwa na woga katika utoaji taarifa za ukiukwaji wa uadilifu. Hata hivyo, taarifa hizo ziwe za kweli si majungu.

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kuthibiti Uadilifu (KKU) SUA, Prof. Christopher Mahonge wakati akizungumza na wafanyakazi katika Kampasi ya Mizengo Pinda iliyoko mkoani Katavi. Amesema utoaji wa taarifa za kweli utasaidia kuyashughulikia malalamiko ya ukiukwaji wa uadilifu ipaswayo ili kuhakikisha sehemu ya kazi inakuwa mahali pazuri na salama kwa kila mfanyakazi.


Mwenyekiti wa Kamati ya Kuthibiti Uadilifu (KKU) SUA, Prof. Christopher Mahonge akifafanua jambo kwenye mkutano na wafanyakazi hawako pichani (Picha na Gerald Lwomile)

Naye Naibu Rasi wa Ndaki kwa upande wa Taaluma wa Kampasi ya Mizengo Pinda, Prof. Anna Sikira, amesema katika kuhakikisha maadili yanafuatwa katika sehemu ya kazi ni muhimu kwa watumishi kuhakikisha wanafuata miongozo mbalimbali ya kazi.

Prof. Sikira amesema miongozo hiyo inajumuisha matumizi ya lugha sahihi katika eneo la kazi, kufika na kutoka kazini kwa wakati, kuingia darasani kwa wakati, kutimiza wajibu, na kuwa na mahusiano mazuri ya kikazi katika eneo la kazi. Hayo ni miongoni mwa mambo muhimu katika kutimiza uadilifu.


Naibu Rasi wa Ndaki kwa upande wa Taaluma wa Kampasi ya Mizengo Pinda, Prof. Anna Sikira akisisitiza juu ya uadilifu kwa wafanyakazi

Katika hatua nyingine mjumbe wa KKU Dkt. Abdul Katakweba, akizungumza na wanafunzi katika Kampasi ya Mizengo Pinda, amewataka wanafunzi hao kuzingatia maadili yakiwemo ya uvaaji mavazi yenye staha kwa wanafunzi wote wa kike na wa kiume. Pia Dkt. Katakweba amewashauri wanafunzi hao kuzingatia kikamilifu masomo yao kwa sababu hicho ndicho kitu kilichowaleta chuoni.



Mjumbe wa KKU Dkt. Abdul Katakweba, akifafanua jambo

 Jengo hili likionyesha muonekanao wa Kampasi ya Mizengo Pinda Mkoani Katavi.


Mwenyekiti wa KKU Prof. Mahonge wa pili kulia akiwa na Naibu Rasi wa Ndaki kwa upande wa Taaluma wa Kampasi ya Mizengo Pinda, Prof. Anna Sikira wa kwanza kushoto na wajumbe wa KKU


Post a Comment

0 Comments