Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini ,TAKUKURU,imeaswa kuongeza Juhudi zaidi katika mapambano dhidi ya rushwa ya ngono nchini.
Hayo yamebainishwa leo Machi,2,2021 jijini Dodoma na Naibu Waziri wan chi,Ofisi ya Rais ,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora,Deogratius Ndejembi wakati akifungua mkutano ,mkuu wa mwaka wa viongozi wa Taasisi ya Kuzuia na kupambana na rushwa nchini [TAKUKURU].
Naibu Waziri Ndejembi amesema pamekuwa na changamoto ya rushwa ya ngono hususan kesi zinazopelekwa mahakamani kufutika juu ya mwanafunzi anapopewa ujauzito hilo ni kutokana na wazazi kutoka pande mbili kuelewana ,kufanya hivyo ni kosa la rushwa ya ngono na ubakaji na ni wajibu kwa kesi zote kuendelea .
Naibu Waziri Ndejembi ametumia fursa kuipongeza TAKUKURU kwa kuleta mafanikio na heshima kubwa katika Taifa la Tanzania
Mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU Brigedia Jenerali John Mbungo amesema katika taarifa ya utendaji kazi ya TAKUKURU katika kipindi cha Mwezi Julai , 2019hadi hadi Juni,2020 utekelezaji wa malengo ya uzuiaji rushwa ulifikia asilimia 89.8% sawa na asilimia 90%.
Aidha,Brigedia Jenerali Mbungo amesema TAKUKURU inazingatia miongozo ya sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa sheria Na.11 ya mwaka 2017,mpango mkakati wa TAKUKURU 2017-2022.
Akitoa neno la shukrani kwa Mgeni rasmi,mkurugenzi wa uzuiaji rushwa TAKUKURU,Sabina Senja amekabidhi zawadi kwa Naibu waziri Ndejembi ikiwa ni pamoja na kitabu cha sheria ya kuzuia rushwa ya mwaka 2017, mkakati wa kitaifa wa kuzuia rushwa awamu ya tatu,Mpango mkakati wa TAKUKURU miaka mitano,mwongozo wa kupambana na rushwa katika taasisi zote pamoja na taarifa ya utafiti wa rushwa ya ngono wa mwaka 2020.
0 Comments