Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii leo Machi 10, 2021 imepokea taarifa ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kuhusu utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo inayogharimu zaidi ya bilioni 10.3.
Akisoma taarifa ya utekelezaji ya Miradi hiyo mbele ya Kamati hiyo, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo amesema Miradi hiyo inatekelezwa katika Taasisi za elimu zilizopo mkoani Arusha.
Amezitaja Taasisi hizo kuwa ni Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) ambayo inatekeleza mradi wa ujenzi wa Maabara Changamano ambayo katika awamu ya kwanza umegharimu jumla ya Shilingi bilioni 2.3 wakati awamu ya pili mpaka sasa inagharimu zaidi ya Shilingi bilioni 5.3.
Dkt. Akwilapo amesema Mradi mwingine wa zaidi ya Shilingi bilioni 5.7 unatekelezwa katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) ni wa ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wa kike ili
Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela ni moja kati ya Taasisi tatu zilizoanzishwa kwa lengo la kuinua na kuleta matokeo bora ya Sayansi, Uhandisi, Teknolojia na Uvumbuzi katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini mwa Jangwa la shara ambapo Taasisi nyingine zipo Nigeria na Burkina Faso.
Katibu Mkuu huyo amesema Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) kinatekeleza Mradi wa ukarabati na upanuzi ambapo ilitengewa kiasi cha Shilingi bilioni 1.5. Mradi huo unatekelezwa ili kuongezeka idadi ya wanafunzi wanaojiunga na chuo hicho kilichoanzishwa mwaka 1978 na pia kukarabati majengo yaliyochakaa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Stanslaus Nyongo ameipongeza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa usimamizi mzuri wa miradi hiyo ambapo amesema Kamati imeridhishwa na taarifa hiyo na hatua za utekelezaji zilizofikiwa.
0 Comments