SUAMEDIA

BREAKING: Bunge lampitisha Dkt. Phillip Mpango Kuwa Makamu wa Rais wa Tanzania

 





Na: Tatyana Celestine

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limempitisha kwa asilimia mia moja aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Philip Mpango kuwa Makamu wa Rais wa Tanzania hivyo  kumpa nafasi ya kushirikiana na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan katika kuliongoza taifa hilo.

Mapema leo machi 30,2021 Rais wa Tanzania, Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan amempendekeza Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango kuwa Makamu wa Rais.

Jina la Mpango limesomwa bungeni mjini Dodoma leo Jumanne Machi 30, 2021 na Spika Job Ndugai aliyeletewa bahasha yenye jina hilo na mpambe wa Rais Samia Suluhu Hassan

Jina hilo liliwekwa katika bahasha mbili ya juu ilikuwa ya kaki na ya ndani ilikuwa nyeupe, Spika Ndugai alianza kusoma nyaraka hiyo ya Rais akirudia rudia maneno ya utangulizi kabla ya kulisoma jina.

Baada ya kusoma jina wabunge walishangilia kwa nguvu  na kumpigia kura za ndio zilizomfanya Dk, Mpango apate ushindi wa asilimia mia moja na kufanikiwa kuwa Makamu wa Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wabunge waliopiga kura ni 363 na wote wamepiga kura ya NDIO, hakuna kura iliyoharibika.

Hatua hiyo ya kumpata Makamu wa Rais  imekuja kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli aliyefariki dunia Machi 17, 2021 na baadaye nafasi hiyo ikachukuliwa na aliyekuwa Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye sasa ni Rais wa Tanzania.

Dkt.Philip Mpango ataapishwa rasmi kushika nafasi hiyo kesho machi 31,2021 saa 9:00 Alasili Ikulu jijini Dodoma.

VIDEO



Post a Comment

0 Comments