Na Gerald Lwomile
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA)
kimewahakikishia wanafunzi wote wanaosoma chuoni hapo katika Shahada za Juu kuwa
kimeweka mazingira mazuri ya kuhakikisha umiliki wa uvumbuzi na ubunifu
unaofanywa na wanafunzi hao unalindwa kisheria
Akizungumza leo Januari 29, 2021 katika
Siku ya Kuyajua Mazingira ya SUA kwa wanafunzi wanaosoma Shahada za Umahili na
Uzamivu, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine upande wa Taaluma Prof.
Maulid Mwatawala amesema hiyo itasaidia mwanafunzi kumiliki kisheria uvumbuzi
na ubunifu wake
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine upande wa Taaluma Prof. Maulid Mwatawala akisisitiza kuhusu jambo wakati akifungua Siku ya Kuyajua Mazingira ya SUA kwa wanafunzi (hawapo pichani) Picha na Vedasto George
“Tumeanzisha kitengo maalumu ili kuhakikisha uvumbuzi na ubunifu unaofanywa na wanafunzi waliofanya tafiti katika SUA unalindwa kisheria” amesema Prof. Mwatawala
Akizungumzia kwa upande wa muda wa
masomo Prof. Mwatawala amewataka wanafunzi hao kuhakikisha wanautumia vizuri
muda wao kwa kusoma kwa bidii na kufanya tafiti ili kuwa miongoni mwa Majalisi
wa Chuo hicho
Awali akimkaribisha Mgeni Rasmi ili
kufungua Siku hiyo ya Kuyajua Mazingira ya SUA Mkurugenzi
wa Kurugenzi ya Uzamili, Utafiti, Uhaulishaji wa Teknolojia na Ushauri wa
Kitalaamu Prof. Erson Karimuribo amesema katika siku za hivi karibuni
kumekuwa na ongezeko la wanafunzi wanajiunga na Shahada za Juu chuoni hapo na
hii ni ishara kuwa Chuo kinatoa wahitimu bora
Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Uzamili, Utafiti, Uhaulishaji wa Teknolojia na Ushauri wa Kitalaamu Prof. Erson Karimuribo akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi
Amesema kwa mwaka huu kumekuwa
na ongezeko kubwa tangia kuwepo kwa wanafunzi 176 mwaka 2016 hadi kufikia
wanafunzi zaidi ya 240 mwaka huu
“Tuna kila sababu ya kulishukuru Baraza la Chuo na Menejimenti kwa ujumla kwa kutupa ushirikiano mkubwa uliowezesha kuwepo kwa ongezeko la wanafunzi na kwa kweli hakuna shaka kabisa baada ya ongezeko kutoka wanafunzi 176 mwaka 2016 hadi kufikia wanafunzi 240 mwaka 2021” amesema Prof Karimuribo
Naye Mratibu wa Masomo ya
Shahada za Umahili na Uzamivu katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Dk.
Akwilina Mwanri akitoa neno la shukrani kwa mgeni Rasmi amesema anayo matumaini
makubwa kuwa wanafunzi waliojinga na Shahada hizo watamaliza Chuo kwa wakati na
kuwa Majarisi wa Chuo hicho
Mratibu wa Masomo ya Shahada za Umahili na Uzamivu katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Dk. Akwilina Mwanri akitoa neno la shukrani
Dk. Mwanri ameongeza kuwa ni
muhimu kwa wanafunzi hao kuhakikisha wanafanya vizuri kwa kusoma kwa bidii na
Chuo kitatoa ushirikiano wa kutosha kwa wanafunzi wote
0 Comments