Na: Vedasto George
Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo SUA kimetakiwa kubuni vyanzo vyake vipya vya mapato ambavyo vitakiwezesha chuo hicho kuweza kujiendesha kikamilifu katika kazi zake za kiutafiti na kitaaluma.
Mwenyekiti Chande amesema kwa sasa Chuo Kikuu cha Sokoine Cha Kilimo SUA kinategemea ruzuku toka Serikalini,Fedha kutoka kwa washirika wa ndani na nje ya Nchi.
Kwaupande wake Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Raphaeli Chibunda amesema kwa sasa chuo kinatekeleza miradi mbambali ikiwemo ukarabati wa miundombinu ya kufundishia, karakana pamoja na maabara ambazo zitawezesha wanafunzi kujifunza kwa vitendo.
Akiwa katika Shamba la Mafunzo Kitengo cha Ufugaji Samaki na Kilimo Mhe. Jaji Chande amesema chuo kinatakiwa kuweka usimamizi wakutosha ili kuhakikisha wanafunzi wote wanaosoma kozi za kilimo na ufugaji wanapata mafunzo muhimu ambayo yatawasaidia pindi watakapo maliza ili waweze kujiajiri na kuisaidia jamii.
Mwnyekiti huyo wa Baraza la Chuo la SUA pia ametembelea Maktaba ya Taifa ya Kilimo, Maabara ya TEHAMA iliyopo Kampasi ya Edward Moringe Sokoine na anatarajia kuendelea na ziara yake leo siku ya Alhamisi Disemba 17 kwa kutembelea Kituo kipya cha Stendi ya Daladala kilichopo eneo la Mafiga mkoani Morogoro.
0 Comments