SUAMEDIA

SUA yashinda Tuzo mbili kwenye “Moro Inspiration Awards”

Na: Tatyana Celestine

Mtangazaji wa Vipindi vya radio wa SUA fm 101 .1 Emmanuel Daudi marufu kama Emma the Best ameibuka mshindi kwa tuzo mbili zilizotolewa na Moro Inspiration Award.



Akizungumza wakati wa kutoa tuzo hizo jana Desemba 20,2020  Afisa Utamaduni Mkoa wa Morogoro Bi. Sophia Kingwai amesema kuwa Tuzo hizo ni kielelezo cha ubora wa kazi ya mtu anayoifanya hivyo kwa mkoa wa Morogoro hatua hiyo imeonesha kukua katika Tasnia ya Habari na Utangazaji.

Aidha amewaasa watangazaji na wamiliki wa vyombo vya habari kutoweka dhana kuwa tuzo hutolewa Dar es Salaam pekee wanachotakiwa ni kuongeza juhudi katika kazi na Tuzo zitawafata popote walipo.

 Kwa upande wake Mtangazaji na Muandaji wa vipindi wa SUAFM Emmanuel Daudi maarufu kama Emma the Best amesema mashindano hayo yamekuwa chachu katika kazi anazozifanya pia ameshukuru Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kwa kumuamini na kumpa nafasi ya kufanya kazi katika kituo chake pia waandaaji wa Tuzo hizo.

Tuzo hizo zilizoandaliwa na Drama Studio mkoani Morogoro ikiwa ni mara ya kwanza Kushindanisha vituo vya utangazaji na washindi walipata tuzo hizo kama zawadi.

Tuzo hizo zimeshirikisha vyombo vya habari mkoani morogoro katika vipengaele vya Mtangazaji Bora wa mwaka 2020, Kipindi Bora cha mwaka 2020  na tuzo hizo zimeenda Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo

 


Post a Comment

0 Comments